Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Katika kuadhimisha juma la Matendo ya Huruma Kanisa la Waadventista Wasabato Ulimwenguni,Idara ya vijana kanisa la Waadventista Wasabato Dodoma kati imeanzisha mpango wa kufanya usafi wa Mazingira katika shule za msingi na sekondari jijini Dodoma zoezi ambalo limekwenda sambamba na kudeki vyoo ,kushona pamoja na kubrashi takriban viatu vya wanafunzi 400 shule ya Sekondari Dodoma .
Akizungumza na Mtandao huu Mkurugenzi wa Chama cha vijana watafuta njia [Pathfinder] Kanisa la Waadventista Wasabato Dodoma kati ,Baraka Christopher Ntalila amesema idara ya vijana kanisani kwa siku ya kwanza imefanya ukarabati wa miundombinu na usafi vyooni katika shule tatu ambazo ni shule ya sekondari Viwandani,shule ya sekondari Dodoma pamoja na Shule Ya Msingi Makole huku matarajio ni kufikia shule 17 .
Pia amesema wanawatumia vijana wenye talanta mbalimbali kanisani ikiwa ni pamoja na talanta za utengenezaji wa sabuni pamoja wenye talanta za ufundi wa ujenzi huku kanisa nalo likichangia zaidi ya laki tano katika ununuzi wa malighafi ikiwa ni pamoja na Saruji na malighafi za kutengenezea sabuni ya chooni ambapo kila shule wanayoitembelea wanaacha lita 20 ya sabuni hiyo.
Hata hivyo,Baraka amezungumzia jinsi zoezi la kushona na kubrashi bure viatu vya wanafunzi katika shule ya sekondari Dodoma lilivyokuwa na mwitikio ambapo takribani wanafunzi mia nne [400]wamejitokeza kushonewa na kubrashiwa viatu vyao huku akizungumzia matarajio ya Juma la Matendo ya huruma kwa baadae ni kufanya matendo ya huruma ya kutoa damu,kuwatembelea wafungwa pamoja kuwatembelea watoto yatima.
Monica Mwakaringa na Frida Mbando ni miongoni mwa wanafunzi wanaosoma katika shule ya Sekondari Dodoma ambapo wao wameelezea kufurahishwa na jambo hilo la pekee ambapo wametoa shukrani kwa Kanisa la Waadventista Wasabato kwa hatua hiyo ya matendo ya Huruma huku wakiguswa zaidi na zoezi la kushonewa na kubrashiwa viatu bure.
Muonekano wa Tundu la choo moja ya shule za serikali jijini Dodoma kabla halijafanyiwa usafi.
Muonekano wa tundu la choo baada ya kufanyiwa usafi.
Mmoja wa vijana wa Chama cha watafuta njia akifanya ukarabati wa sakafu,mlango pamoja na samani za shule Ya Sekondari Viwandani jijini Dodoma .
Vijana wa Umoja wa Wanafunzi wa Kiadventista Wasabato [ASSA]Shule ya Sekondari ya Dodoma wakuingana na Chama cha Watafuta njia [Pathfinder]Kanisa la Waadventista Wasabato Dodoma kati katika ushonaji wa viatu.
Post A Comment: