Happy Lazaro, Arusha.
Serikali imeahidi kutatua changamoto kubwa inayokikabili kiwanda cha usindikaji wa maziwa cha Kilimanjaro fresh cha jijini Arusha ,kinachokabiliwa na changamoto ya ukubwa wa kodi ya ongozeko la thamani ambayo inachangia kushindwa kufikia uzalishaji mkubwa wa maziwa kama uhitaji wake ulivyo .
Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha maziwa cha Kilimanjaro Freshi jijini Arusha ,Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ullega amesema kwamba serikali kupitia wizara yake itahakikisha inaondoa changamoto hiyo ya tozo kwa lengo la kuimarisha uzalishaji wa usindikaji wa maziwa katika kiwanda hicho .
Ulega amesema kuwa, kiwanda hicho toka kuanzishwa kwake kimekuwa na mafanikio makubwa ambapo aliwataka kununua kwa bei kubwa zaidi kwa wafugaji ambao wataweza kuzalisha zaidi na kuongeza thamani ya uzalishaji .
Amesema kuwa ,kitendo cha kununua kwa bei kubwa kwa wafugaji kitatoa motisha zaidi ya wafugaji kuendelea kuzalisha zaidi na hatimaye kuweza kuongeza uzalishaji wa maziwa kwenye kiwanda hicho.
Aidha aliwataka kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wafugaji hasa kuhusu uzalishji ulio bora na kwa kisasa ili waweze kuondokana na changamoto mbalimbali huku akiwataka kuandika bar us ya malalamiko hayo ili yaweze kufanyiwa kazi haraka kwa faida ya sekta ya maziwa nchini.
Awali akitoa maelezo ya Kiwanda hicho Mkurugenzi wa kiwanda hicho cha Kilimanjaro Fresh kilichopo mjini hapa,Irfhan Virjee alimweleza Naibu waziri changamoto zinazo mkabili katika uzalishaji wa maziwa kuwa ni tozo ya kodi ya vat ambapo aliomba iondolewa.
Amesema kuwa ,wanatarajia kuzalisha lita zipatazo elfu 20 ambapo wanatarajia kuanza kuuza maziwa nje ya nchi ambapo walianza kuzalisha lita 3,000 na hadi sasa wanazalisha lita 8,000 kwa siku.
Virjee amesema kuwa,kiwanda hicho kimekuwa mkombozi kwa wafugaji kutoka vyama vya ushirika ambapo huwauzia maziwa kwa kiasi cha shilingi 800 hadi kufikia shilingi 850 ambapo wakulima hupatiwa motisha kwa lengo la kuendelea kutunza mifugo kwa lengo la kuboresha mifugo kupata maziwa yaliyo na ubora wa hali ya juu .
Mwisho.
Post A Comment: