Na Ferdinand Shayo, Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefungua mkutano wa Mawaziri wanaosimamia sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii kutoka nchi za Jumuiya Maendeleo kusini mwa jangwa la Sahara (SADC) uliofanyika jijini Arusha .
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo amezitaka nchi za SADC kuweka mikakati na kuridhia itifaki ya mazingira ili kutunza mazingira na kuweka jitihada za pamoja za kuhifadhi mazingira ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira.
“Kazi ya Kuhifadhi na kulinda mazingira yetu ni yetu wenyewe" Anaeleza Makamu wa Rais akifafanua umuhimu wa kutunza mazingira.
Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali zinasubiri mapendekezo yanayotokana na mkutano huo kwa ajili ya utekelezaji kwa maslahi mapana ya SADC na nchi wanachama.
Nae Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla amesema kuwa Mawaziri hao watapitisha mapendekezo ya kuwa na mkakati wa pamoja wa kupambana na ujangili na kuhakikisha kunakua na utalii endelevu.
Pia tutaangalia itifaki ya SADC Kuhusu usimamizi wa misitu, itifaki ya mpango wa maendeleo ya utalii kwa nchi zote.
Majadiliano yanaendelea Mkutano wa Sekta za Mazingira, Maliasili na Utalii utahitimishwa jioni ya leo.
Post A Comment: