Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro amewataka wakazi wa Arusha kuhakikisha kuwa wanawapeleka watoto wakapate chanjo ya ugonjwa wa surua na polio ili waweze kuwakinga watoto wao na magonjwa ya moyo ,kifua kikuu pamoja na ulemavu unaoweza kuzuilika.

Akizungumza katika uzinduzi wa Chanjo katika jiji la Arusha uliofanyika katika kituo cha afya cha Levolosi ,Daqqaro amesema kuwa chanjo hizo zitatolewa kwa watoto kuanzia miezi 9 mpaka miaka 5 ni salama na zinalenga kuwasaidia wananchi kuwa na kinga dhidi ya magonjwa ili kujenga taifa lenye wananchi wenye afya bora watakaoweza kuchangia katika maendeleo ya jamii na taifa .Ha

Gabriel amesema kuwa serikali imeweka msisitizo kuhusu suala la chanjo ambalo lina umuhimu mkubwa na litatolewa katika vituo vya afya na zahanati ambazo zimeteuliwa kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo muhimu.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dr.Saimon Chacha amesema timu ya wataalamu imejipanga kuhakikisha chanjo inawafikia watoto wote walioko kwenye jiji la Arusha hivyo amewataka wananchi wa Arusha kujitokeza kwa wingi.

Chacha amesema kuwa chanjo hiyo itatolewa bure kwa wananchi kwani serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wametoa chanjo hiyo muhimu kwa ajili ya watoto.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: