Waziri
wa nchi,Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Seleman
Jafo ametoa agizo kwa Wakuu wa Mikoa,na Makatibu tawala wa Mikoa kote
nchini kuhakikisha wanasimamia vyema mpango kazi wa Taifa wa uendelezaji
wa Miji ili kuepuka ukuaji wa Makazi Holela.
Waziri Jafo ametoa Maagizo hayo jijini Dodoma wakati wa Uzinduzi wa Mpango kazi wa wa Taifa wa Maendeleo ya Miji Tanzania .
Waziri
Jafo amesema suala la mpango kazi wa Maendeleo ya Miji Tanzania itakuwa
ajenda ya Kitalii na itakuwa na faida kubwa ikiwa ni pamoja na urahisi
wa huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na kupitikika kwa maeneo kwani
amesema kuna baadhi ya Mitaa haipitikiki kutokana na Makazi holela hali
ambayo husababisha hata magari ya zimamoto kushindwa kutoa huduma
vizuri.
“Unakuta
nyumba zimekaa kiholela hata gari la zimamoto linashindwa kutoa huduma
vizuri na hali ambayo inasababisha kuteketea kwa watu pamoja na
mali,maeneo mengine ni ya kusikitisha sana hata kupitisha jeneza ni
shida ,Bila shaka kuna Vijana wengine hapa wana Magari Mazuri lakini
wanayaengesha nyumba ya ng’ambo kwa jirani kisa hapapitiki”Alisema
Hivyo
Waziri Jafo amesema katika kuhakikisha mpango kazi wa Maendeleo ya Miji
Tanzania unafanyika bila vikwazo vyovyote ameagiza Wakuu wa Mikoa na
Makatibu tawala wa Mikoa kote nchini kusimamia vyema ili kuleta ufanisi
Mzuri katika utekelezaji wake.
Naibu
Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema
moja ya hatua ambayo Wizara imefanya ni pamoja na kupitia Sera ya
Makazi ya Taifa ya mwaka 2000 na kupanga sera Mpya ya Nyumba lengo
likiwa ni kupunguza Umasikini na Kukuza Uchumi pamoja na Kuboresha
huduma za kijamii.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi [ESRF]Dkt.Tausi Kida amesema
Mnamo Agosti ,2017 Serikali ya Tanzania iliungana na Taasisi hiyo
kuanzisha Maabara ya ukuaji wa Miji Tanzania kwa lengo la kusaidia
serikali katika uchambuzi mbalimbali wa ukuaji miji huku Naibu katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Adolf Ndunguru akishukuru ushiriki wa
Taasisi hizo.
Post A Comment: