Zikiwa zimebaki siku 57
kufikia Tamasha kubwa la utalii hapa Nchini linalo fahamika kama “Swahili
International Tourism Expo” ,Bodi ya utalii Tanzania TTB imethibitisha kuwa imejipanga
vema kuwapokea wageni toka nchi 60 watakaoshiriki Tamashahilo.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari Jijini Dar es Salaam leo , Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii, Devotha Mdachi
ameeleza kuwa Tamasha hilo litafanyika oktoba 18 hadi 20 mwakahuu, katika Kumbi
za Mikutano Mlimani City, huku mawakala zaidi ya 200 wakitarajiwa kushiriki katika
Maonyesho hayo.
Hata hivyo, Devotha amesema
juhudi za kufanikisha ujio wa wageni hao zaidi ya 200 kutokaNchi 60 zimefanywa kwa
ushirikiano mkubwa kutoka Bodi ya Utalii TTB pamoja na Balozi zetu mbalimbali za
nje.
“mpaka sasa tumepokea uthibitisho
kutoka ofisi za ubalozi; toka nchi mbalimbali zikiwemo Ubalozi wa Sweden, Ubalozi
wa Tanzania Nchini Malaysia, Ubalozi wa Tanzania Nchini China, Ubalozi wa Korea
yaKusini, Ubalozi wa Japani, Ubalozi wa Kanada,
Ubalozi wa Afrika Kusini, Ubalozi wa Omani, Ubalozi wa India, Ubalozi wa Uingereza, Ubalozi wa Brazili” Amezitaja Mkurugenzi Devotha.
Akieleza zaidi juu ya upokeaji
wa wageni hao watakaofika katika Tamasha hilo, amesema wamejipanga na kujiboresha
zaidi kwa kuwapeleka katika maeneo mbalimbali ya utalii nchini, ikiwemo Hifadhi
ya Wanyama Serengeti, Uduzungwa, Mikumi, FukwezaTanga, Mapango ya Amboni, Mlima
Kilimanjaro, Miradi ya Utalii wa Utamaduni mikoa ya Arusha na Kilimanjaro,piavisiwavya
Zanzibar na Mafia.
Sambamba na hilo, kampuni
na Mashirika mbalimbali zaidi ya 30 yamejitolea kuunga mkono juhudi hizo zinazo
fanywa na TTB katika kuelekea kilele cha Maonesho hayo.
“kampuni kuu ambazo tayari
zimetoa udhamini ni The Global Vector Control Standard, Benki ya CRDB ambayo ni
mdau mkubwa katika sekta ya Utalii pamoja na shirika la Ndege la Ethiopia”
Mkurugenzi alitaja wadhamini
wetu wakiwemo ni Air Tanzania, Hifadhi ya Taifa TANAPA, Mamlaka ya Hifadhi ya NgoroNgoro,
Mamlaka ya Wanyama Pori Tower, Wakala wa Misitu TFS, na vyama vya Utalii.
Post A Comment: