Diwani Baraka Simon diwani wa kata
ya Olturoto kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), amechaguliwa kuwa
Makamu Mwenyekiti, halmashauri ya Arusha, baada ya kuchaguliwa na
wajumbe wa Baraza hilo, na kupata nafasi ya kuliongoza Baraza hilo kwa
kipindi cha mwaka mmoja 2019/2020.
Akitangaza motokeo ya uchaguzi huo,
Mkurugenzi mtendaji, halmashauri ya Arusha, Dk. Wilson Mahera, amesema
kuwa kura zilizopigwa ni 33, na hakuna kura iliyoharibika, Mheshimiwa
Abert Oltulele amepata kura 13 na mheshimiwa Baraka Simon, amepata kura
20.
"Kwa mamla niliyopewa ninamtangaza
mheshimiwa Baraka Simon kuwa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha
kwa kipindi cha mwaka mmoja" amesema Mkurugenzi huyo.
Makamu Mwenyekiti mheshimia Simon,
amechukua nafasi hiyo baada ya kupata kura 20, na kumshinda mpinzani
wake mheshimiwa Albert Oltelele, diwani wa kata ya Oloirien kutoka chama
cha CHADEMA aliyepata kura 13 kati ya kura 33 zilizopigwa.
Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Makamu
Mwenyekiti huyo mpya, licha ya kuwashukuru wajumbe hao, ameahidi
kufanyakazi kwa ushirikiano na wajumbe wote, kwa lengo la kuwatumikia
wananchi wa halmashauri ya Arusha.
Aidha mheshimiwa Makamu Mwenyekiti,
amewasihi madiwani wote kushirikiana bila kujali tofauti zao za vyama,
na kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kama ilivyowasilishwa na
mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli
wakati wa kuingia madarakani mwaka 2015.
Hata hivyo uchaguzi huo umefanyika
kulingana na Kanuni, sheria na taratibu za kuongoza Baraza la Madiwani,
kila baada ya mwaka mmoja, kuchagua Makamu Mwenyekiti wa Baraza la
Madiwani.
Post A Comment: