Na Eric Msuya -  MAELEZO
Zikiwa zimebaki siku 57 kufikia Tamasha kubwa la utalii hapa Nchini linalofahamika kama “Swahili International Tourism Expo” , Bodi ya utalii Tanzania TTB imethibitisha kuwa imejipanga vema kuwapokea wageni toka nchi 60 watakaoshiriki Tamasha hilo. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari  Jijini Dar es Salaam leo , Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii, Devotha Mdachi  ameeleza kuwa Tamasha hilo litafanyika  oktoba 18 hadi 20 mwaka huu, katika Kumbi za Mikutano Mlimani City, huku  mawakala zaidi ya 200 wakitarajiwa kushiriki katika Maonyesho hayo. 

Hata hivyo, Devotha amesema juhudi za kufanikisha ujio wa wageni hao zaidi ya 200 kutoka Nchi 60 zimefanywa kwa ushirikiano mkubwa kutoka Bodi ya Utalii TTB pamoja na Balozi zetu mbalimbali za nje. 

“mpaka sasa tumepokea uthibitisho kutoka ofisi za ubalozi; toka nchi mbalimbali zikiwemo Ubalozi wa Sweden, Ubalozi wa Tanzania Nchini Malaysia,  Ubalozi wa Tanzania Nchini China, Ubalozi wa Korea ya Kusini,  Ubalozi wa Japani, Ubalozi wa Kanada, Ubalozi wa Afrika Kusini, Ubalozi wa Omani, Ubalozi wa India,  Ubalozi wa Uingereza,  Ubalozi wa Brazili” Amezita Mkurugenzi Devotha 

Akieleza zaidi juu ya upokeaji wa wageni hao watakaofika katika Tamasha hilo, amesema wamejipanga  na kujiboresha zaidi kwa  kuwapeleka katika maeneo mbalimbali ya utalii nchini, ikiwemo  Hifadhi ya Wanyama Serengeti, Uduzungwa, Mikumi,  Fukwe za Tanga, Mapango ya Amboni, Mlima Kilimanjaro, Miradi ya Utalii wa Utamaduni mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, pia visiwa vya Zanzibar na Mafia. 

Sambamba na hilo, kampuni na Mashirika mbalimbali  zaidi ya 30 yamejitolea kuunga mkono juhudi hizo zinazofanywa na TTB katika kuelekea kilele cha Maonesho hayo. 

“kampuni kuu ambazo tayari zimetoa udhamini ni  The Global Vector Control Standard, Benki ya CRDB ambayo ni mdau mkubwa  katika sekta ya Utalii … pamoja na shirika la Ndege la Ethiopia” 

Mkurugenzi alitaja wadhamini wetu wakiwemo ni Air Tanzania … Hifadhi ya Taifa TANAPA, Mamlaka ya Hifadhi ya NgoroNgoro, Mamlaka ya Wanyama Pori Tower, Wakala wa Misitu TFS, na vyama vya Utalii.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: