Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini Eliezer Rweikiza akitoa ufafanuzi kuhusiana na Bima ya Kilimo katika maonyesho ya 26 Kanda ya kaskazini Njiro Mkoani Arusha.
 Paulo Makanja ni Mwanasheria Mwandamizi kutoka TIRA:amesisitiza wakulima wanaodai malipo ya Bima wafike banda la TIRA kwaajili ya msaada zaidi
 Meneja wa TIRA kanda ya Kaskazini Eliezer Rweikiza akisisitiza kwajambo mteja kama anavyoonekana katika picha,kushoto kwake ni Paulo Makanja ni Mwanasheria Mwandamizi kutoka TIRA 
Na.Vero Ignatus,Arusha

Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini TIRA imepitisha na kutoa mwongozo wa Bima ya kilimo ikiwa na maana ya kusisitiza wananchi ambao wanajihusisha na kilimo kwenda  katika maonyesho ya 88 ili waweze kupatiwa huduma ili kukinga kilimo chao na mifugo yao .


Eliezer Rweikiza ni Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini amesema kuwa yapo makampuni ambayo ni mahususi kwa huduma hiyo na siyo makampuni yote yanatoa huduma ya kilimo na mifugo .


Amesema hivi karibuni  Mamlaka hiyo imeendesha mafunzo  kwenye vikundi takribani 50vinavyojumuisha VICOBA,SACOS,AMCOS, pamoja na wajasiriyamali ambao wamejipanga kujieleza jinsi ya kupata hizo huduma za kilimo

 Ameainisha vijiji ambavyo wametoa elimu kwa ujumla kwa mkoa wa Tanga Mjini vipo 10.Muheza 12,Korogwe 11,Babati 6,na Hanang 8.

Rweikiza mesema huduma hizo zimekuwa zikutolewa zaidi ya miaka mitano nyuma ila kwa sasa zinakuwa na vitu ambavyo vimeboreshwa zaidi kwani zipo huduma hadi kwa wakulima wadogo

Rweikiza amesema kuwa mkulima anapokata bima ya kilimo inamkinga na majanga kwani mkulima akipata hasara anafidiwa na kampuni husika vilevile mkulima anakuwa amekinga uchumi wake hakiti nje ya ulingo unabakia palepale

Kahiyo hii bima ni muhimu sana kwa wote wanaolima kilimo kikubwa au kilimo kidogo ,yote haijalishi huduma  ya bima ipo inahusika ,kwahiyo tunawataka sana wananchi hasa kanda ya kaskazini wakate bima ya Kilimo na Mifugo

Paulo Makanja ni Mwanasheria Mwandamizi kutoka TIRA amesema kuwa katika msimu huo wa nanenane watashughulika na malalamiko ya wananchi amabapo wanayadai makampuni mbalimbali ya bima ambapo madai yao hayaja shughulikiwa hadi sasa,na kuwasaidia namna gani wanaweza kulipwa madai yao yale yanayolipika.

Sambamba na hayo amesema kuwa watashughulika namna ya kutoa ushauri kwa kwa watu ambao wanahitaji kusajili makampuni yao katika kufanya shughuli za Bima,kwa maana ya wale wanaohitaji kufanya udalalali,Mawakala,sambamba na wale wanaotaka kufanya kazi ya ukadiriaji hasara za Kibima

Amesema kuwa miongozi mwa kazi kubwa ya mamlaka hiyo ni kuhakikisha kuwa masoko ya Bima linakuwa linaendeshwa kwa uhuru,wazi, faida kwa watu amabao ni wanufaika katika shughuli za Bima.

Ametoa wito kwa wakazi wa kanda ya kaskazini kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo kwani wamegundua ya kwamba uwelewa wa bima bado haujawa mkubwa hivyo wananchi watembelee banda la TIRA sambamba na mabanda mengine yanayojihusisha  na shughuli za bima katika mtaa wa Bima.

Maonyesho hayo ni ya 26 yaKilimo na sherehe za nanenane yanayoendelea Themi Njiro Mkoani Arusha yamebeba kauli mbiu isemayo: Kilimo,Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa Uchumi wa Nchi

Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: