Mwandishi wa habari wa kujitegemea, Erick Kabendera leo Agosti 5, 2019 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka matatu.

Kabendera amesomewa mashtaka matatu ambalo ni kujihusisha na mtandao uwa uhalifu, kukwepa kulipa kodi, utakatishaji fedha kiasi cha Shilingi 173, 247,047.02.

Hati ya Mashtaka yanayomkabili Erick Kabendera;



Julai 29, Taarifa kuhusu kutoweka kwa Mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera zilienea nchini.

Kulikuwa na utata wa awali kuhusu iwapo ilidaiwa ametekewa na watu wasiojulikana kama ilivyo kwa baadhi.

Julai 30, 2019, Polisi nchini Tanzania ilisema kuwa mwanahabari wa Erick Kabendera aliyedaiwa kutoweka hakutekwa bali amekamatwa.

Kamanda wa polisi kanda maalum ya mji wa Dar Lazaro Mambossasa amesema polisi wanafanya uchunguzi kuhusu uraia wa mwandishi huyo kwa ushirikiano wa idara ya uhamiaji kabla ya kumwasilisha mahakamani.

Siku mbili baadaye, Idara ya uhamiaji ilithibitisha kuwa inamshikilia Kabendera kutokana na kuwa na mashaka na uraia wake, kamishna wa uraia na mdhibiti wa pasipoti, Gerald Kihinga alithibitisha.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: