NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAONESHO ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es
Salaam, tayari yamepamba moto ambapo Mkurugenzi wa Banda la Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, ametoa
wito kwa Wanachama wa Mfuko huo pamoja na Wananchi kufika kwenye banda hilo
ili kupata elimu kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko.
Bi. Chiume amesema, banda la PSSSF liko jengo
namba 13 mkabala na jengo la matangazo ndani ya viwanja vya Maonesho
Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
"Mfuko wa PSSSF umeundwa baada ya kuunganishwa
kwa mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya GEPF, PSPF, LAPF
na PPF na kwa sababu hiyo bado ni mpya na wanachama wanahitaji kuelimishwa
kuhusu majukumu mapya ya Mfuko huo kwa wanachama ambao ni watumishi wa
Umma." Alifafanua Bi. Chiume.
Alisema uduma za PSSSF zitatolewa kwenye jingo
moja ambalo pia linatumiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii
(NSSF).
Maonesho hayo yameanza Juni 28 na yatafikia
kilele Julai 13, 2019 na kauli mbiu ya mwaka huu ni "Usindikaji wa Mazao ya
Kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda."
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. William Erio (kushoto), akizungumza na
Mkurugenzi wa Banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma
(PSSSF), Bi. Eunice Chiume (wapili kushoto), pamoja na Afisa Matekelezo wa
NSSF, Bi.Diogi Janguo, (wapili kulia) na Mtaalamu wa mifumo ya computer,
NSSF Bi.Grace Magigile wakati Bw. Erio alipofika kwenye jengo namba 13
ambalo Mifuko yote miwili ya PSSSF na NSSF inatoa huduma kwa ushirikiano
katika jengo hilo. Itakumbukwa kuwa PSSSF ni Mfuko ulioundwa kuhudumia
Watumishi wa Umma na NSSF kuhudumia Sekta binasi.
Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw.
Donald P. Maeda (kushoto), akimuhudumia Mwanachama wa Mfuko
huo.
Afisa Mwandamizi wa Malipo, Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma,(PSSSF), Bi.Nyangi Masalu (kulia),
akiwahudumia wanachama wa Mfuko huo waliotembelea banda la PSSSF kwenye
viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam Juni 30, 2019.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF,
Bw. Abdul Njaidi (kushoto), akiwahudumia wananchi hawa waliofika kwenye
banda hilo.
Timu ya PSSSF ikiongozwa na Mkurugenzi wa Banda
la Mfuko huo Bi. Eunice Chiume ikiwa tayari kutoa huduma bora kwa wanachama
na wananchi watakaofika kwenye banda hilo.
Post A Comment: