NA MWANDISHI WETU, MWANZA
MKUTANO wa 23 wa Taasisi zinazosimamia Mawasiliano kwa Nchi za Afrika Mashariki, (EACO) umeanza leo Julai 1, 2019 jijini Mwanza.
Sambamba na mkutamno huo pia wajumbe watashiriki
Mkutano Mkuu wa 26 wa EACO ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kuiweka
Afrika Mashariki katika eneo la Uchumi wa Kidijitali".Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye, ndiye aliyefungua mkutano huo utakaodumu hadi Julai 5, wenyeji ni Tanzania, pamoja na mataifa mengine ya WAC, ambayomni Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wapili kushoto), akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasilkiano Tanzania (TCRA), Mhandisi James M. Kilaba (watatu kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya (TCRA), Dkt. Jones Killimbe (wanne kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa EACO Dtk. Ally Yahya Simba(wakwanza kulia) na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Mawasiliano Bw.Mulembwa Munaku. (wakzwanza kushoto), baada ya kufungua mkutano wa 23 wa Taasisi zinazosimamia Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO), utakaofuatiwa na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 26 wa EACO jijini Mwanza Julai 1, 2019
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James M. Kilaba, akizungumza na waandishi wa habari kufafanua baadhi ya mambo kuhusu mkutano huo.
Wajumbe wenyeji Tanzania, wakimsikiliza Mhe. Naibu Waziri Mhandisi Nditiye wakati akifungua mkutano huo.
![]() |
Mhe. Naibu Waziri Mhandisi Nditiye na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka mataifa wanachama wa EACO. |
Post A Comment: