Mmoja wa makaka mapacha wenye utata nchini Zimbabwe wanaofahamika kama Fichani twins, ambao waliwahi kugonga vichwa vya habari kwa kukukusanya umati wa watu katika mitaa ya mji mkuu wa Zimbabwe Harare mwaka 2006 walipovaa vipande vya ngozi ya mbuzi zilizoficha tu sehemu zao za siri amedai kuwa amekwishalala na wanawake zaidi ya 1000.

Gazeti la New Zimbabwe limeripoti kuwa Tafadzwa Fichani ambaye kwa sasa anaishi katika eneo la kati nchini humo la Gokwe Nembudzi ameliambia kuwa kwa sasa anaishi na virusi vya HIV na sasa ni mgonjwa wa Ukimwi na hivyo hajali kwa kiasi kwamba hatumii kinga yoyote ya kuzuwia maambukizi hayo.

"Ni kwanini nitumie mipira ya kondomu wakati sasa ninafahamu kuwa nimeathirika na HIV, nijilinde ili iweje sasa?" Tafadzwa aliuliza huku akijigamba.

Tafadzwa ni mchimbaji wa madini , akiendesha biashara zake katika eneo lenye shughuli za uchimbaji madini la Zenda na anajivunia tabia yake ya kuwatumia wanawake atakavyo.

" Nimelala na zaidi ya wanawake 1000. Kile ninachoweza kukwambia ni kwamba wanawake hawajali muonekano wa sura, kile wanachoitaka ni pesa ," Tafadzwa aliliambia gazeti la New Zimbabwe.com na kuongeza kuwa amekuwa muathiriwa wa utajiri wake.

" Pesa zangu zote nilizopata kutokana na madini, nimezitumia kuwafurahisha wanawake na hicho ndicho wanawake wanachokitaka. Pesa hapa sio tatizo.''
Share To:

msumbanews

Post A Comment: