![]() |
Afisa Utamaduni wa Manisp[aa ya Sumbwanga Kiheka Charles a.k.a K Chars. |
Katika kuunga mkono na kuieleza jamii juu ya juhudi
zinazofanya nwa serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Dkt. John Pombe
Magufuli, Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Sumbawanga Kiheka Charles a.k.a K
Chars ameibuka na wimbo wa kuelezea mazuri yanayofanywa na serikali ya
Tanzania.
Katika kueleza malengo ya kutunga wimbo huo alioupa jina
la Mchaka Mchaka na kumshirikisha msanii Mackpaul Sekimanga a.k.a Makamua, K
Chars alisema kuwa kama kiongozi na mshauri wa wasanii ni jukumu lake kuwaonesha
wasanii mada mbalimbali za kuimba na sio kujikita kuyaimbia mapenzi wakati
wanaweza kuimba kuhusu kuhamasisha lishe bora, kuhimiza kilimo cha mazao
mbalimbali na faida zake, kukemea mimba za mashuleni, ndoa za utotoni,
kuboresha huduma za afya nakadhalika.
"Hakuna msanii wa nje atakayekuja kusifu nchi yetu
isipokuwa sisi wenyewe kusifia maendeleo yetu na kuyatangaza kwa wengine, hivyo
nikaona niyaweke katika wimbo mazuri yaliyofanywa na serikali ambayo jamii
inapaswa kuyafahamu, msanii ana nafasi kubwa ya kusikilizwa na jamii na yapo
mengi ya kuyazungumzia katika maisha yetu, hivyo ni vyema wasanii wakajielekeza
katika kuhamasisha mambo ya kimaendeleo, kuyaimba mazuri ya serikali na
kuyaibua yale ambayo wanaona serikali inahitaji kuyafahamu ili yafanyiwe
kazi," Alisema
Halikadhalika, alisifu juhudi za Mkurugenzi wa Manispaa
ya Sumbawanga, James Mtalitinya, kwa kumuunga mkono katika juhudi za kuibua
vipaji vya wasanii wa Sumbawanga tangu kuanzishwa shindano la "Sumbawanga
Talent Search" lililowahusisha wasanii wa kuimba, hadi kumalizika kwa
shindano hilo.
Katika Shindalo hilo ambalo fainali yake ilifanyika usiku
wa mkesha wa Mwenge wa Uhuru 2019 na mshindi wa kwanza alipata shilingi
300,000/=, wa pili 200,000/= na wa tatu 100,000/= na walioingia kwenye kumi
bora wamepewa fursa ya kurekodi wimbo wa kuelezea fursa za uwekezaji
zinazopatikana katika Mkoa wa Rukwa pamoja na kusifu ukarimu wa watu wa mkoa
huo, kibao kinachotarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi July,2019.
K Chars ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi mbalimbali
wa mkoa kuwasaidia na kuwaunga mkono wasanii wachanga wanaoutangaza mkoa.
Post A Comment: