Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo(MB) (Kulia) akitoa maelekezo wakati wa ziara yake aliyoifanya jana Jijini Arusha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo(MB) ( kushoto) akiwa katika moja ya chumba cha kutolea huduma za afya katika Kituo cha Afya Kaloleni
Na Fatuma S. Ibrahimu – Arusha Jiji 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo(MB) amepongeza ujenzi wa barabara ya oljoro murriet inayojengwa kupitia mradi wa TSCP awamu ya tatu wenye gharama ya Shilingi Bilioni 22. 3 inayojengwa na mkandasi kutoka kampuni ya Sinohydro Co-Operation Ltd ya nchini China.

Mhe. Jaffo ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake Jijini Arusha mapema leo hii alipotembela mradi huo wa ujenzi wa barabara unaosimamiwa na mhandisi wa barabara wa Jiji Eng. Agust Mbuya na kujionea hatua nzuri iliyofikia ujenzi huo ambapo kwa sasa upo kwenye hatua za awali na unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 11 mwaka 2019 na kuanza kutumiwa na wananchi.

“Nichukue fursa hii kukupongeza mhandisi kwa usimamizi mzuri wa ujenzi huu, pia nitoe rai kwa mshauri elekezi wa ujenzi wa mradi huu kufanya kazi kwa niaba ya halmashauri , kushauri kwa weledi na kuwa mtetezi mkuu kwa upande wa Serikali kwani atakapokuwa upande wa mkandarasi basi Halmashauri itashindwa kufikia malengo kwani itakosa mshauri mwenye kusimamia haki ” Alisema Mhe. Jaffo.

Sambamba na ziara yake hiyo kwenye mradi wa ujenzi wa barabara Mhe. Jaffo pia alitembelea kituo cha afya cha Kaloleni kilichopo Jijini hapa ili kujionea matumizi ya kiasi cha Fedha shilingi milioni 400 zilizotolewa na Serikali tagu tarehe 26 June, 2018 kwa ajili ya kukarabati majengo katika Kituo hicho pamoja na ujenzi wa wadi mbalimbali.

"Nimepokea barua nyingi kutoka hapa kutaka mbadilishe matumizi ya ujenzi wa majengo ya hospitali pamoja huduma za meno ,sitaki mbadilishe chochote hapa na jumatano kazi ianze na nitakuja kukagua mwenyewe ukamlishwaji wa jengo hili novemba 30 mwaka huu " alisema Mhe. Jafo.

Pia Waziri Jafo alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqqaro kufuatilia na kuhakikisha ujenzi wa jengo hilo unaanza Jumatano wiki ijayo. 

Naye Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dk. Simon Chacha alimhakikishia Waziri Jaffo kuwa wataanza ujenzi wa majengo ya upasuaji na wodi ya wazazi, jengo la X Ray, sehemu ya Kusubiria wagonjwa (waiting bay),Jengo la kufulia na ukarabati wa chumba cha meno, dawa, Maabara na mfumo wa maji taka katika kituo hicho cha Kaloleni ili kuboresha huduma za afya.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: