Diwani Viti maalumu Mhe. Sikitu Sanziyote, ameendelea kuwajengea uwezo wajasiriamali wa kata zote 18 za halmashauri ya Jiji la Mwanza. Akiwa kata ya Mhandu amekabidhi hati nne za usajiri kwa vikundi vya Umoja wa Wanawake Kata ya Mhandu, Kikundi cha Mtaa wa Shigunga shina 4, Shina namba 5 pamoja na namba 6 ambavyo vinakamilisha idadi ya vikundi 44 ambavyo ameviwezeshwa fedha taslimu 30,000 ya usajiri, 20,000 ya ufunguaji wa kitabu cha Bank kwa kila kikundi".
Mhe Sanziyote amevihasa vikundi hivyo kutumia umoja huo vizuri katika kujikwamua kiuchumi, kujiwekea akiba na kutumia fursa za mikopo kukuza mitaji. Kadharika amemshukuru Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanislaus Mabula kwa ushirikano wake, Uliowezesha utoaji wa mafunzo ya ujasirimali na uandikaji wa katiba katika mchakato wa uhamasishaji wananchi na wajasirimali wajiunge katika vikundi.
Naye Mhe. Constantine Sima diwani mwenyeji alitumia adhara hiyo kumpongeza Mhe. Sanziyote kusaidia usajiri pamoja na mafunzo vikundi vya wajasirimali kata ya Mhandu. Hafla hiyo ilihudhuliwa na Mhe. Donata Yusuph Gappi Diwani kata ya Mkuyuni, Viongozi wa CCM kata ya Mhandu.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Post A Comment: