Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubeba amesema hana mpango wa kuhamia CCM kutokana na madhira aliyoyapata.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 30, 2018 Kubenea amesema hana sababu hata moja ya kuipenda CCM.

“Mimi siondoki humu kama kuna mambo ya kurekebisha ndani ya chama nitarekebisha nikiwa humu. Nikishindwa kurekebisha nitaacha na kufanya shughuli zangu kwa sababu mimi ni mwandishi wa habari, nitarudi kwenye kazi zangu."

Kubenea amefafanua kuwa wanaofanya mchezo huo mchafu wa kuchafuana ni vijana wa Chadema.

Kuhusu kushutumiwa na chama amesema kuna taratibu ikiwamo kuitwa kwenye kamati ya maadili kitu ambacho hajawahi kufanyiwa.

"Nashutumiwa vipi na sijawahi hata kuhojiwa na kamati yoyote,"

Amesema yeye ni mbunge kwa miaka mitano, hivyo atakuwa na Chadema kwa muda wote labda Mungu aichukue roho yake.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: