Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kuivusha Yanga wakati wa mpito, Abbas Tarimba, ametangaza kuachana rasmi na wadhifa huo.

Kwa mujibu wa Radio Uhuru, Tarimba amefunguka na kueleza kuwa kumekuwa hakuna maelewano baina yake na Makamu Mwenyikiti wa Yanga, Clement Sanga, ambaye ameivunja kimyakimya kamati hiyo ambayo ilipitishwa katika mkutano mkuu.

Kufuatia tukio la kuvunjwa kwa kamati, Tarimba amesema hawezi akawa na muda wa kuonana na Sanga kwasababu ameivunja kamati, na hata kama asingefanya hivyo asingekuwa tayari kutekeleza majukumu ya kamati hiyo.

"Waachane na mimi , mimi sina muda wa kuonana na Sanga waachane na mimi, yeye kwanza kamati kaisha ivunja na hata kama wasinge vunja mimi nisingeweza kufanya kazi nao" alisema Tarimba.

Mbali na kauli hiyo, Tarimba amekanusha uwepo wa taarifa zilizokuwa zimeripotiwa kuwa kamati yake imelipa madeni ya fedha zote zilizokuwa ni malimbikizo ya madeni kwa wachezaji.

Tarimba ameeleza kuwa hakuna ukweli kuhusiana na hilo akiwahusisha viongozi wa Yanga kuwa wamekuwa waongo hivyo na kuwaomba waache masuala ya usanii kwa kuwa klabu hiyo ni taasisi kubwa.

"Wanayanga mnadanganywa Yaani wanayanga mnadanganywa mchana kweupe, Yanga tuna tamaduni zetu sio hizi, viongozi ni waongo ,nawaomba watulize akili zao wasaidie timu ,wengine ni wakubwa wanaongoza mpaka bodi ya ligi ,sasa watumie ukubwa huo kuipeleka Yanga mbele waache uongo uongo" alisema
Share To:

msumbanews

Post A Comment: