Kikao cha 35, mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea Bungeni mjini Dodoma muda huu, likiwa limeongozwa Naibu Spika wa Bunge,Tulia Ackson,Ambapo kipindi cha maswali na majibu kiliendelea; Tazama matukio katika picha

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe.Dkt.Tulia Ackson akitambulisha wageni wa jukwaa la Spika wakati wa kikao cha thelathini na tano cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma

Rais wa Umoja wa Vijana wa Bunge la Afrika na Mbunge wa Handeni Vijijini Mhe.Mboni Mhita akitoa shukurani mbele ya Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania toka achaguliwe kuongoza umoja huo ivi karibuni nchini Afrika ya kusini ambapo atatumikia kwa muda wa miaka mitatu

Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika na Mbunge na Mbunge wa Shinyanga Mjini Mhe.Stephen Maselle akitoa shukurani mbele ya Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania toka achaguliwe kuongoza Bunge hilo ivi karibuni nchini Afrika ya kusini

Wanafunzi wa Sekondari ya Huruma ya Jijini Dodoma(kushoto) na Wanachuo wa Chuo cha Diplomasia(kulia) wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt.Augustine Mahiga akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 leo Jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt.Augustine Mahiga na Naibu wake Mhe.Dkt.Suzan Kolimba wakipitia hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kabla ya kuwasilisha leo Jijini Dodoma

Mbunge wa Viti Maalum Mhe.fatma Toufiq(CCM) akiuliza swali kutaka kujua mpango wa Serikali kudhibiti hali ya wanafunzi kupewa ujauzito na waendesha bodaboda leo Jijini Dodoma
Share To:

msumbanews

Post A Comment: