Na George Mganga
Kikosi cha Ndanda kimesafiri mpaka jijini Mwanza kwa ajili ya mechi na Mbao FC katika Ligi Kuu Bara.
Ndanda ambayo imekuwa haina maendeleo mzuri msimu huu inakutana na Mbao ambayo pia inawania kujikwamua kuteremka daraja.
Walima korosho hao wa Mtwara, wamekuwa dhoofuli hali ambapo hadi sasa wamejikusanyia jumla ya pointi 23 wakiwa nafasi ya 15 kwenye msimamo na wakiwa wamecheza michezo 27.
Wapinzani wao watakaokuwa wenyeji wa mechi hiyo, Mbao FC nao wana hali ngumu kwa kuwa na tofauti ya alama moja mbele ya Ndanda.
Mbao ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 24 huku wakicheza jumla ya michezo 26 ya ligi.
Mchezo wa leo unaweza ukatoa taswira mbaya zaidi kwa Ndanda endapo itakubali kuachia alama tatu muhimu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Vilevile Mbao itakuwa imejiwekea mazingira mazuri zaidi ya kuendelea kusalia katika Ligi Kuu Bara endapo itashinda mchezo wa leo.
Post A Comment: