Haruna Niyonzima.
KOCHA wa Simba, Pierre Lechantre amesema ugumu wa mechi wanazokutana nazo kwa sasa ndiyo sababu kubwa inayomfanya kutowatumia kabisa Haruna Niyonzima na Said Ndemla katika mechi mbili zilizopita.
Niyonzima ambaye hivi karibuni alitoka katika kipindi cha majeraha, hajawa sehemu ya kikosi cha Simba ambacho kimecheza dhidi ya Prisons na kushinda mabao 2-0 na dhidi ya Mbeya City waliyoshinda kwa mabao 3-1. Mechi zote zilichezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Championi Jumatano, Lechantre amesema ameshindwa kuwatumia viungo hao kwenye mechi hizo mbili kwani wapinzani wao walikuwa wanakaba sana na kutumia nguvu nyingi.
“Kuhusu Niyonzima kutocheza nilifanya hivyo kwa sababu kwenye mechi hizi mbili ambazo tumecheza na Mbeya City na Prisons, nilibaini kwamba wapinzani wangu wana watu ambao wanacheza kwa nguvu kubwa sana.
“Pia watu wao wanakaba sana hivyo nikaona nisiwatumie viungo halisi wanaocheza nafasi ya kiungo mchezeshaji na nikawapanga watu wengine.
“Kama mechi na Prisons utaona kabisa wapinzani wetu walikuwa wanacheza kwa kukaba mtu na mtu, sasa hapo ningesema kwamba nitumie viungo wachezeshaji ambao kwenye suala la kukaba siyo wazuri ingekuwa pigo kwetu hivyo nilichofanya ni kuwaweka pembeni tu.
“Lakini kwenye michezo ijayo wanaweza kutumika kwani siyo kila mchezo ambao tutacheza mambo yatakuwa hivihivi,” alisema Lechantre raia wa Ufaransa.

Post A Comment: