Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekanusha taarifa zilizodai kuwa Mkurugenzi wa CZI, Cyprian Musiba amefukuzwa Bungeni.

Taarifa hizo ziliibuka mara baada ya kuwepo picha mtandaoni ikimuonyesha Musiba ‘akizozona’ na baadhi ya watumishi wa Bunge. Kupitia ukurasa wa Twitter wa Bunge wamefafanua kuhusiana na hilo;
Picha zinazosambaa kwenye mitandao zikidai kuwa Mkurugenzi wa CZI Ndg. Cyprian Musiba amefukuzwa Bungeni si kweli. Musiba amekidhi vigezo vya kusajiliwa kuripoti habari za Bunge na kwamba alikuwa akihamishwa kwenda katika jukwaa mahsusi ambalo Waandishi hukaa wawapo Bungeni.
Musiba ni Mhariri wa Gazeti la Tanzanite na Mwanasheria, hivi karibuni alifunguliwa kesi na Mjasiriamali/Mwanahabari na Mkurugenzi wa Compass Communications, Maria Sarungi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa madai ya kumkashifu na kuchafua jina lake kupitia mkutano wake na Waandishi wa Habari uliyofanyika February 25, 2018.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: