Wasichana zaidi ya 17,840, Mkoani Iringa wanatarajiwa kupata chanjo ya Saratani ya Mlango wa Uzazi ifikapo mwishoni mwa mwezi April mwaka huu.
Mratibu wa Afya Mkoani humo, Naftali Mwalongo, amebainisha hayo wakati wa kikao cha uzinduzi wa kamati ya uhamasishaji Mkoani Iringa kuwa chanjo ya HPV itatolewa kwa awamu ikiwa na lengo la kutoa kinga kwa watoto wa kike wenye umri kati ya miaka 9 hadi14.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Lukas Kambelenje, amesema ni mara ya Kwanza chanjo ya HPV kufanyika Mkoani humo,
Aidha ameitaka Kamati hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuhamasisha wazazi kuwapeleka watoto wao kupata Chanjo hiyo
Post A Comment: