Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Simba Sports Club, Haji S. Manara, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na klabu ya Al Masry ya Nchini Misri inayotarajiwa kutua hapa nchini kesho.

Klabu ya Simba inatarajia kucheza mchezo wake wa Kombe la Shirikisho dhidi ya klabu ya Al Masry kutoka nchini Misri siku ya Jumatano ya tarehe 7/3/2018 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza mishale ya saa 12 kamili jioni, Aidha viingilio katika mchezo huo vinataraji kuwa katika bei zifuatavyo;-

  1.             VIP A – Tsh 20000
  2.             VIP B –  Tsh 15000
 III.            Mzunguko/Orange – Tsh 5000.

Tiketi za kuingilia uwanjani siku hiyo zitaanza kuuzwa siku ya Jumatatu kwa mawakala wa Selcom na vituo vitakavyotangazwa hapo baadae.

Klabu inawaomba mashabiki na wapenzi wa klabu kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuishangilia timu yao itakapokuwa inacheza, aidha inawakumbusha kununua tiketi za mechi hiyo kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Klabu ya Al Masri  inataraji kuwasili nchini siku ya Kesho Jumapili majira ya saa 12 jioni,na itafanya mazoezi siku ya Jumatatu jioni katika Uwanja wa Taifa.

Pia,waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Afrika kusini wanatarajia kuwasili nchini siku ya Jumatatu saa 10 jioni.
Imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano,

Simba Sports Club,
Haji S. Manara
3/3/2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: