Kutoka Venezuela usiku wa kuamkia leo March 29, 2018 watu zaidi ya 70 wameuawa baada ya moto kuzuka kwenye moja ya magereza yenye wafungwa wengi zaidi nchini Venezuela.

Moto huu ulifuatiwa na jaribio la wafungwa wa gereza hilo kutaka kutoroka. Inaelezwa kuwa moto huo ulianza baada ya wafungwa kuchoma magodoro ili kutoroka.
Maaskari wametumia gesi ya machozi ili kuwasambaratisha ndugu mbalimbali wa wafungwa na raia wengine waliokuwa wamezunguka gereza hilo wakifanya vurugu ili kujua kuhusu majeruhi na waliokufa kama ni ndugu zao.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: