Rais wa TFF, Wallace Karia hii leo amezungumzia hajira alizotowa katika kipindi ambacho ameingia madarakani mpaka sasa.

AJIRA
Katika kipindi changu cha uongozi (Kamati ya Utendaji) kwa kushirikiana na ofisi ya Katibu Mkuu tumeweza kupunguza wafanyakazi kutoka Wafanyakazi 44 tuliowakuta wakati naingia madarakani hadi kufikia 21,Ni hatua kubwa na tunafanya upembuzi makini kabla hatujaanza kuajiri watu tuwe na mahitaji stahiki.
KATIBU MKUU
Kumekuwa na maneno mengi juu ya nafasi ya Katibu Mkuu wa Shirikisho, Ndugu zangu wakati naanza kazi niliona ni muhimu nafasi hii ikaimishwe kwa mtu anayelijua shirikisho vizuri na ambaye sina shaka na uwezo wake,Sifa zote hizi alikuwanazo KIDAO WILFRED na wajumbe wa Kamati ya utendaji chombo ambacho kinahusika nakupitisha kilibariki awe Kaimu Katibui MKuu.
Kutoka nje ya Ofisi na kukaimu hii siyo mara ya kwanza,wakati Ndugu Tenga anashinda Uraisi alimuomba Bi.Lina Kessy ambaye alikuwa mtumishi wa Serikali kuwa Mratibu wa Ofisi, nafasi iliyokuwa kama Mkuu wa sekretarieti wakati huo.
Hata wenzetu wa CAF, Rais ndiye anayepeleka jina bila kujali Mchakato utakavyokuwa kwa maana wanaweza wakatangaza au wasitangaze,na hata Katiba ya TFF inahitaji Rais wa TFF atoe mapendekezo ya Katibu Mkuu ili Kamati ya Utendaji ijadili, haya yanafanyika kwa sababu Rais kama msimamizi wa Sekretarieti anafanya kazi kwa karibu sana na Katibu Mkuu hivyo FIFA wanahitaji watu hawa  wawe wanaoweza kufanya kazi kwa karibu sana,ndipo Rais wa TFF anapopewa kipaumbele cha mtu wa kufanya naye kazi kwakuwa ndio nguzo ya Taasisi kwakuwa Rais ndio mkuu wa Taasisi na Katibu Mkuu ndio mkuu wa Sekretarieti.
Lakini pamoja na yote hayo bado nilikuwa napeleka ajenda ya Ajira kwenye Kamati ya Utendaji ili kushauriana njia bora ya kupata Katibu Mkuu kwa maslahi mapana ya Mpira wa Miguu na siyo mtu.
Niwahakikishie kikao kijacho cha kamati ya Utendaji kitaamua njia sahihi ya kupata Katibu Mkuu na tutahakikisha tunakuwa na Katibu Mkuu ndani ya muda mfupi ujao.
Mipango Mbalimbali
Tumekuwa katika Ujenzi wa Mipango Mbalimbali kama nilivyoainisha kwenye Ilani yangu ambapo Katibu Mkuu amekuwa Kiungo muhimu katika kunisaidia kwenye Ujenzi wa Mipango yangu hiyo lakini kwa bahati Mbaya Kaimu Katibu Mkuu Kidao amekuwa kwenye wakati mgumu kutokana na kuandamwa na Maneno na Vitendo vinavyolenga na kufanikisha kumkwamisha na kumkosesha mazingira bora na rahisi ya kufanyia kazi zake na hivyo imekuwa ni atahri kwa TFF kwa Baadhi ya Mipango yake kuwa inakwama kutoka Mpaka sasa na hiyo ni athari kwa Mpira wetu kwa Ujumla.
Ndugu zangu jambo la pili ambalo nimeona niligusie ni jinsi vyombo vya maamuzi vya TFF vinavyofanya kazi,
Ndugu waandishi, TFF inafanya kazi kwa mujibu wa Katiba yake ya mwaka 2013 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2015. Katiba hii inataja Kamati ya Utendaji itaundwa na Wajumbe wafuatao;
1. Rais
2. Makamu wa Rais
3. Wajumbe 13 kutoka kanda zilizotajwa ibara 32 ya katiba ambazo ni Kanda namba 1-Kagera na Geita
Kanda namba 2- Mara na Mwanza
Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu
Kanda namba 4- Arusha na Manyara
Kanda namba 5- Kigoma na Tabora
Kanda namba 6- Katavi na Rukwa
Kanda namba 7- Mbeya, Iringa na Songwe
Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma
Kanda namba 9- Lindi na Mtwara
Kmada namba 10- Dodoma na Singida
Kanda namba 11- Pwani na Morogoro
Kanda namba 12- Kilimanjaro na Tanga
Kanda namba 13- Dar es Salaam
4. Wajumbe wawili wanowakilisha vilabu vya Ligi Kuu
5.Mwenyekiti wa Chama cha Soka ya Wanawake.
6. Mwenyekiti wa Kamati ya Tiba
7. Wajumbe wawili wa kuteuliwa na Rais wa TFF.
Rais wa TFF amepewa nafasi za kuteua wajumbe wawili wa kamati ya Utendaji ili kumsaidia kufanya kazi na watu ambao wanajua muelekeo wake lakini ambao anaamini watamsaidia kwenye maeneo mbalimbali katika Taasisi.
Kamati ya Utendaji inafanya kazi na vyombo mbalimbali ambavyo ni Kamati ndogondogo, Bodi ya Ligi na Kamati za Kisheria pamoja na Kamati za Uchaguzi.
Kamati Ndogondogo;
 1. Fedha na Mipango
 2. Mashindano(Kamati ya Tuzo na Soka la Ufukweni)
 3. Ufundi na Maendeleo
 4. Vijana
 5. Wanawake
 6. Waamuzi
 7. Katiba, Sheria, na Hadhi za wachezaji.
 8. Tiba
 9. Ukaguzi (ambayo yenyewe ni kama Kamati huru)Kamati za Kisheria;
 1. Nidhamu
 2. Rufani ya Nidhamu
 3. Maadili
 4. Rufani ya Maadili
Kamati za Uchaguzi;
 1. Uchaguzi
 2. Rufani ya Uchaguzi
Ufanyaji wa kazi wa Kamati hizi umeelezewa katika Katiba ya TFF kwa maana Kamti za Kisheria zinajitegemea huwa haziingiliwi kwenye maamuzi yake.Ingawa vikao vyake vyote huwa vinaratibiwa na ofisi ya Katibu Mkuu.
Kwahiyo maamuzi ya Kamati hizi huwa ni ya kujitegemea hivyo watu wote ambao wamekuwa wanahukumiwa na Kamati hizi ni vyema wakawa wanajua utaratibu wa Kamati zinavyofanya kazi.Na mimi binafsi nimeendelea kuheshimu Kamati zifanye kazi bila kuingiliwa na mtu yoyote vile.
Ndiyo maana wakati nachaguliwa niliahidi kusimamia Taasisi kwa uadilifu mkubwa bila kumuonea aibu mtu yeyote, wala kumuogopa mtu na hii ni katika kuunga mkono juhudi za Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ya kupambana na uchafu  wa aina zote katika serikali,Nami nimeamua kusafisha Taasisi kama nilivyoahidi wakati wa Kampeni za uchaguzi ulioniweka madarakani,niseme wazi hakuna mtu asiye muadilifu atabaki katika mpira,Na nimpongeze  Kaimu Katibu Mkuu wangu kwa kusimamia kwa ujasiri mkubwa usimamiaji wa maagizo yote halali ya Kamati mbalimbali,Amekuwa anasimamia bila uoga bila kujali anavyosakamwa kwangu linanipa faraja sana.
Tumekuwa tunachukuwa hatua katika kila eneo tumeshaanza kuchukuwa hatua kwa wizi wa Mapato ya milangoni, kuna viongozi wamefungiwa,hatukuishia hapo tayari viongozi walioghushi leseni za usajili wamefungiwa,Hiyo yote ikiwa ni kuonesha sina masihara hata kidogo kwenye kuhakikisha mpira unakuwa sehemu ya watu waadilifu.
FIFA walituma Timu ya Uchunguzi(Investigation Team) kuangalia yale yote yaliyofanyika toka mwaka 2013 mpaka mwaka 2017,Timu ilikaa nchini kwa takribani wiki mbili ikifanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Katibu Mkuu,Yaliyogundulika yameacha doa kubwa na walitoa Ripoti na Maelekezo ya mambo ya kuyafanyia kazi na ya kuchukulia hatua.
Masharti yote haya yaliambatana na kuzuiwa kwa fedha zetu za miradi nia na wenzetu wachache, Lakini tumekosa pesa zinazoitwa Operation Cost ikiwa ni shinikizo la Dola Milioni Tatu ambazo tulipaswa kulipwa toka mwaka 2015-2018.
Karibia nchi zote Duniani zimenufaika kwa kupata pesa hizi, isipokuwa Tanza kuhakikisha tunatekeleza masharti ya FIFA, Hivyo tulipopata ripoti tumeamua kutekeleza kwa asilimia mia moja maagizo yote ya FIFA. Haya yanayotokea ni Miongoni mwa Matokeo ya Utekelezaji wa Taarifa za Wakaguzi wa TFF na Wakaguzi na Timu ya Uchunguzi kutoka FIFA. Jambo hili limepitia Hatua stahiki kwa Mujibu wa Taratibu zinazohusiana na Taarifa za kiUkaguzi na wahusika wameshirikishwa ipasavyo na Utetezi wao walipeleka kwenye Kamati husika ya Ukaguzi miezi iliyopita baada ya kutakiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa taratibu.
Niseme tu unaposafisha Taasisi kuna gharama zake TFF inahitaji Kuungwa Mkono zaidi kwa Hatua Madhubuti inazochukua za Kujisafisha na Kusonga Mbele.
Katika VITA hii ya Kupambana na Udhalimu kwenye Mpira wetu Hatutarudi Nyuma, Tutapambana bila hofu wala woga almuradi Hakuna dhulma wala Uonevu wala Upendeleo kwa yeyote. Na Nitoe wito kama kuna Kiongozi au Mdau yoyote anayejua ana Pesa za TFF kinyume cha Utaratibu Natoa WITO Ajisalimishe Mwenyewe.
Ahsanteni kwa kunisikiliza naamini mtaniunga mkono ili kuusogeza mbele Mpira wa Tanzania.
Mwisho niwakumbushe TFF inaendelea na maandaalizi ya Matayarisho wa AFCON U 17,2019 .Timu ya ukaguzi ya CAF itakuja mwezi wa Tano, tumekuwa tunalifanyia kazi kwa ukaribu  na serikali kuhakikisha changamoto za viwanja vitavyochezea mashindano pamoja na viwanja vya mazoezi vinakuwa tayari kwa wakati.Tutaendelea kulitolea ufafanuzi kila wakati.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: