MWANACHAMA na shabiki wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ pamoja na viongozi wa timu hiyo wanapanga mipango madhubuti ya kuhakikisha wanawazidi kete wapinzani wao Yanga kwa kutwaa ub­ingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, ambapo kwa kulifaniki­sha hilo wametenga pembeni kiasi cha Sh milioni 100.

Iko hivi, Simba na Yanga kwa sasa wote wanalingana pointi kwenye msimamo wa ligi kuu wak­iwa na 46 kila mmoja ambapo vita baina yao inaonekana kuwa kubwa kutokana na kila timu kupanga ka­rata zake vyema wakati huu ambao ligi inaenda mwishoni.

Kwa sasa Simba ambao wenyewe wanaongoza kwa tofauti ya ma­bao, wamebakiza mechi 10 pekee kabla ya kumalizika kwa ligi ambapo uongozi wa timu hiyo umepanga kuwapa milioni 10 wachezaji wake kwenye kila mchezo ambao wa­takuwa wanashinda kwa ajili ya kuongeza hamasa ya kufanikisha jambo hilo.

Katika mechi hizo 10 zilizobakia, wachezaji wa Simba watavuna milioni 100 kama watashinda mechi zote ikiwemo ya watani wao Yanga iliyopangwa kupigwa Aprili 7, mwaka huu ambapo fedha hizo milioni 5 watatoa viongozi wengine huko 5 akitoa Mo, hadi mwisho wa ligi Mo atakuwa ametoa milioni 50.

Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Simba, Haji Manara, alisema: “Huu ni mkakati wa kuongeza hamasa kwa wachezaji wetu kuipambania timu yao kutwaa ub­ingwa wa ligi kwa msimu huu baada ya kuukosa kwa misimu kadhaa nyuma.

“Kiasi hicho cha fedha kitakuwa kinatolewa na makao makuu ambao watatoa milioni 5 kwa kila mechi huku mwekezaji wetu Mo Dewji yeye katika mechi hizo naye atachangia milioni 5, hivyo ukichanganya zote hapo unapata milioni 10 kwa kila mchezo.

“Tena itakuwa mzigo unaingia muda mfupi tu baada ya kumaliza mchezo, kama ikitokea mechi ni Jumapili basi Jumatatu asubuhi hivi kila mmoja atakuwa ameingiziwa fungu lake benki, tunafanya yote haya kwa ajili ya kuonge­za hamasa kwa wache­zaji,” alisema Manara.

Naye kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amefungukia juu ya michezo yao hiyo 10 iliyobakia am­bapo alisema: “Mechi hizi 10 zilizobakia siyo nyingi sana, kikubwa ambacho tunataki­wa kukifanya ni kuende­lea kupigana tupate pointi kwa kila mechi.”
Share To:

msumbanews

Post A Comment: