Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amefunguka na kusema kuwa yeye hana uhakika kama mwanadada mwanaharakati wa mitandaoni Mange Kimambi kama ni binadamu wa kawaida kama yeye. 
Tulia Ackson amesema hayo alipohojiwa na moja ya chombo cha habari na kusema kuwa kwa sasa hawezi kusema kama mwanadada huyo anakosea au laa kwa kuwa hana uhakika kama yupo kama yeye na kusema labda akipata fursa ya kuonana naye na kuona kweli yupo kama yeye ndiye anaweza kuwa na la kusema. 
"Sina hakika kama yeye ni binadamu wa kawaida kama mimi kwa hiyo sijui labda nikikutana naye ndiyo nitajua chakuzungumza naye lakini kwa yale nayoyasikia hapa na pale sina hakika kama yeye ni binadamu wa kawaida kama mimi ila kama yupo kama mimi basi nitapata fursa ya kumshauri nikionana naye, siwezi kusema anakosea kama nilivyosema sijajua yeye ni mtu wa namna gani kwa hiyo huenda hakosei labda ni aina yake ya binadamu yaani ni specie tofauti hivyo kama yeye ni specie ya tofauti huwezi kusema anakosea"alisema Tulia Ackson 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: