Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Abdul Nondo anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha jana usiku majira ya saa 5 hadi 6 akiwa jijini Dar es Salaam. 
Chanzo cha karibu cha mwanafunzi kikiongea na eatv kimesema kuwa Abdul Nondo mpaka saizi haifahamiki yupo wapi na namba zake za simu pia hazipatikani toka jana usiku. 
Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa jana mwanafunzi huyo alituma ujumbe mfupi  uliokuwa ukionyesha yupo kwenye hali ya hatari na baadae namba yake haikupatikana tena hivyo hawajui yuko wapi mwanafunzi huyo. Mwandishi wa eatv alipojaribu kupiga namba hizo pia zilikuwa hazipatikani 
Feb 18, 2018 Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Abdul Nondo alimtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba kujiuzulu nafasi yake hiyo kutokana na kushindwa kuangalia mienendo ya jeshi la polisi nchini, lakini pia kiongozi huyo aliitaka siku nne zilizopita aliwataka TAHLISO waache kuwa wasemaji wa wizara na serikali na wakumbuke majukumu yao mazito ya kusemea wanafunzi wa vyuo vikuu kwa sababu wanalipishwa ada vyuo vikuu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: