Mshindi wa zabuni ya uwekezaji ndani ya klabu ya Simba Mohammed Dewji amesema klabu ya Al Masry ya Misri wamesalimika kufungwa na Simba kwasababu walikuwa wanajiangusha.

Simba imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kutoka suluhu ugenini dhidi ya Al Masry usiku wa kuamkia leo.

Mo Dewji kupitia Ukurasa wake wa Twitter amesema Al Masry wamepata bahati tu kutokana na muda mwingi kujiangusha lakini Simba walitawala mchezo.

Simba imetolewa baada ya kuruhusu sare ya mabao 2-2 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam wiki mbili zilizopita hivyo Al Masry kusonga mbele kwa mabao ya ugenini.

Simba sasa imebaki na michuano ya ligi kuu soka Tanzania Bara pekee baada ya kutolewa kwenye kombe la shirikisho nchini mapema hatua ya 64 bora na Green Warriors.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: