Meneja wa mafunzo wa Sunking ,Immaculate Shija (Kushoto)akikabidhi baadhi ya misaada walioutoa kwa mkurugenzi wa kituo cha Nice Orphance Center,Florida Christian baada ya kutembelea
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya sunking wakishusha misaada mbali mbali ikiwemo vyakula
Hii ndio Misaada iliyotolewa na kampuni ya umeme wa sola (sunking )Kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Nice Ophance Center kilichopo Bwawani wilayani Arumeru kilometa 35 kutoka jijini Arusha
KAMPUNI ya kusambaza Umeme wa Sola Majumbani ya Sunking Mkoa wa Arusha imekabidhi msaada wa Tenki la kuhifadhia maji lenye ukubwa wa lita 3000,vyakula pamoja na mtambo wa umeme wa Sola kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Nice Orphance Center kilichopo katika kijiji cha Bwawani wilaya ya Arumeru,mkoani Arusha.
Akikabidhi msaada huo wenye thamani ya sh,milioni 6,leo machi 31,meneja Mafunzo wa kampuni hiyo, Immaculate Shija amesema kuwa msaada huo ni sehemu ya faida kidogo wanayoipata na kuamua kuirejesha kwa jamii ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao katika masuala ya maendeleoo ya kijamii
Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo hicho cha kulelea watoto yatima ,Florida Christian amesema kuwa kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2006 na hadi sasa kinawatoto wapatao 44 na kimekuwa kikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa majengo ya kuwatunzia watoto,fedha za kuwasomesha pamoja na mahitaji mengine ya watoto hao.
Kampuni ya Sunking ni moja kati ya kampuni zinazofanya vizuri katika kuyaangaza maisha kupitia umeme wa sola na imefanikiwa kufunga mitambo zaidi ya 50,000 katika vijiji vilivyoko katika mikoa 26 iliyoifikia hapa nchini.
Post A Comment: