Shirika la umeme mkoani Rukwa limeendesha zoezi la bomoabomoa kwa wakazi wa Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa waliojenga kwenye njia kuu ya umeme wa msongo mkubwa unaotoka nchi jirani ya Zambia.

Zoezi hilo lililofanyika chini ya usimamizi wa shirika hilo limewakumba wakazi wa mtaa wa Eden katika Manispaa ya Sumbawanga ikiwa ni baada ya hatua za kisheria kukamilika.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga amesisitiza umuhimu kwa wakazi wa Manispaa hiyo kufuata taratibu za ujenzi ili kuepuka hasara ya namna hiyo, baadhi ya wakazi wa eneo ilipoendeshwa bomoabomoa wamekiri ukiukwaji wa sheria.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: