Teddy A na Bam Bam
Watu wanaofuatilia shindano la Big Brother Naija watakuwa wanaelewa kuwa shindano hilo kwa sasa mambo ni Moto Moto kwani awali lilianza kuboa na baadhi ya watu walianza kulidharau kwa kulinganisha na lile lililozoeleka la nchini Afrika Kusini.
Jana usiku wa kuamkia leo washiriki wawili Teddy A na mpenzi wake Bam Bam ambao wanapewa nafasi kubwa kuibuka washindi kwenye shindano hilo, waliibua mijadala mitandaoni baada ya kunaswa na kamera wakifanya mapenzi bafuni.

Hata hivyo mchezo huo mchafu haukuishia bafuni kwani walivyotoka waliendelea pia kuvunja amri hiyo kitandani ambapo Teddy A alionekana kwenye video akiwa juu ya Mrembo Bam Bam.

Hata hivyo watu wengi wamekosoa tabia za washiriki wa Big Brother Naija 2018 kwa kujihusisha na mapenzi zaidi na ku’FAKE’ maisha kuliko kuonesha uhalisia.
Hii ni mara ya pili kwa tukio hilo baada ya washiriki Miracle na Nina kujihusisha na ngono wiki iliyopita, na tayari watu wengi wameanza kumlaumu Biggie kwa kukaa kimya juu ya vitendo hivyo.
Shindano la Big Brother Naija mwaka 2018 ni la tatu kufanyika, na limeanza mwezi Januari 28, mwaka huu ambapo mshindi atakabidhiwa kitita cha Naira milioni 45 sawa na Tsh milioni 283.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: