Wizara ya madini imesema kuwa itashirikiana kwa karibu sana na Chama cha wauza madini nchini hapa kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanajadiliana kwa pamoja ili waweze kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wauzaji  madini hao.

Naibu waziri wa Madini,Doto Biteko aliyasema hayo juzi alipokuwa akizungumza katika kikao cha pamoja na wauzaji wa madini nchini kilichofanyika  jijini Arusha

Amewaagiza maofisa wa Wizara hiyo kuhakikisha kuwa wanaondoa ukiritimba katika utoaji wa vibali vya kazi na kwamba wavitoe haraka pindi taratibu zinapokamilika na kwamba kusiwe na ubaguzi wa aina yeyote ule katika shughuli za madini.

Amesema kuwa serikali kipitia Wizara yake inaendelea kushugulikia migogoro ya mipaka katika migodi ambayo imedumu kwa muda mrefu lengo ni kuhakikisha kuwa suluhu inapatikana na shughuli za uchimbaji zinafanyika kwa amani.

Naibu Waziri huyo amewataka wachimbaji na wauzaji wote wa madini waliopata mikopo kutoka katika Wizara hiyo kuhakikisha kuwa wanairejesha mapema ili itumike kuwakopesha wengine na atakayekiuka atachukuliwa hatua kali za kisheria.

 hoja za wachimbaji wadogo wakati na wale wakubwa zitafanyiwa kazi huku kilio chao kikubwa ni kuhusu sheria mpya ya madini ambayo imefanyiwa maboresho hivi karibu kuhusu uzaji na uchimbaji wa madini ya tanzanite pamoja na dhahabu

kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha wauza madini Tazania TAMIDA Thomas Munisi amesema kuwa wamefuraishwa sana na majibu ya naibu waziri kutambua changamoto zinazo wakabili na kuahidi kuyafanyia kazi, amesema Rais Magufuli amefanya uteuzi mzuri kwani manaibu waziri hao wamekua wasikivu kusikia kilio cha wauza madini hapa nchini

Munisi amesema kuwa wanaunga mkono hatua ya Serikali ya kutaka madini yote yanayochimbwa kufanyiwa hatua zote zinazohitajika hapa nchini kwa lengo ya Tanzania ya viwanda kutimia kwani hali hiyo itachangia ongezeko la ajira kwa vijana wa kitanzania. 

Makamu mwenyekiti huyo amewasihi wauza madini wote hapa nchini kuhakikisha kuwa wanazingatia yale yote waliyojadili katika mkutano huo na kuhakikisha kuwa wanafanyia kazi maagizo ya Serikali ili waweze kushirikiana zaidi katika shughuli hizi za madini.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: