Naibu waziri wa maji,Bwana Juma Aweso akiteta jambo na katibu wake mara baada ya kupokea taarifa ya Halmashauri ya wilaya ya Singida inayohusu sekta ya maji.
kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida,Faustine Kiyui akisoma taarifa ya sekta ya maji ya Manispaa ya Singida kwa Naibu waziri wa maji,Bwana Juma Aweso.
Naibu wazziri wa maji,Bwana Juma Awesso akiongozaa kikao cha watendaji wa Halmashauri ya wilaya na Manispaa ya Singida baada ya kupokea taarifa za Halmashauri hizo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Ni baadhi ya watendaji wa serikali wa wilaya ya Singida wakiwa katika kikao cha pamoja na Naibu waziri wa maji,Bwana Juma Aweso kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Singida.


NAIBU Waziri wa maji,Juma Aweso amewaagiza wataalamu wa maji nchini kuwasimia kwa karibu wakandarasi waliopewa kazi za miradi ya maji katika suala zima la utekelezaji wa miradi hiyo na kuwaahidi kwamba wizara hiyo haitaweza kuwa kikwazo katika kuhakikisha wakandarsi hao wanalipwa fedha zao kwa wakati ili miradi hiyo isikwame.

Naibu Waziri huyo alitoa agizo hilo mjini Singida wakati wa ziara yake ya siku moja Mkoani Singida kutembelea na kukagua baadhi ya miradi ya maji iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida.

Aidha Aweso alisisitiza kwamba katika ziara zake anazoendelea kufanya amebaini kwamba matatizo ya upatikanajai wa huduma ya maji safi na salama haiwezi kupatikana kwa wataalamu wa wizara hiyo kukaa ofisini kwa kuchezea kompyuta,bali maji yanapatikana kwa wananchi kutokana na kuwatembelea wananchi na kubaini kero zao.

“Na tunafanya ziara tukitambua kabisa maji hayapatikani kwa kukaa ofisini kwa kuccheze kompyuta,maji yanapatikana kwa wananchi kwa sababu anayelala na mgonjwa ndiye anayejua mihemo ya mgonjwa.”alifafanua Naibu Waziri huyo.

Hata hivyo Aweso aliweka bayana kwamba akiwakatika ziara yake ya wiki moja Mkoani Shinyanga alibaini baadhi ya miradid iliyokuwa ikisuasua lakini baada ya kuisukuma imeanza kwenda vizuri na hivyo kutumia fursa hiyo kuwaahidi wananchi wa Mkoa wa Singida kwamba anatarajia kurudi Mkoani hapa kufanya ziara katika Halmashauri zote za Mkoa wa Singida.

Kwa mujibu wa Aweso lengo la ziara hiyo Mkoani Singida ni kuhakikisha kuwa miradi inayosuasua inapata msukumo ili mwisho wa siku ile azma ya wananchi kuhakikisha wanakwenda kutuliwa ndoo kichwani,inatekelezeka kama ambavyo Rais Dk.John Pombe Magufuli alivyoahidi.

Akizungumzia changamoto alizokumbana nazo katika Mkoa wa Singida,Naibu Waziri huyo aliweka bayana kwamba katika mji wa Singida bado wananchi wanakabiliwa na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama,jambo ambalo linatakiwa litafutiwe ufumbuzi wa kina na wa haraka zaidi.

Naibu huyo wa Waziri hata hivyo alibainisha kwamba kiwango upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katikaa Mkoa wa Singida ni asilimia 44 kwa wananchi wa mjini wakati azma ya rais ni kwamba ifikapo mwaka 2020,kiwango kifikie asilimia 95 kwa mjini na asilimia 85 kwa maeneo ya vijijini.

“Kwa hiyo serikali imetoa fedha sisi tunachoitaka Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Singida (SUWASA) inatangaza tenda kwa haraka ili wananchi wa Singida waweze kupata maji lakini kikubwa uzingatie Mkandarasi atakayepatikana ni yule mwenye uwezo katika kuhakikisha mradi hausuisui ili wananchi hao waweze kupata maji safi na salama”alisisitiza Naibu Waziri huyo.

Akimkaribisha Naibu Waziri huyo,Mkuu wa wilaya ya Singida,Eliasi Tarimo alisama ziara ya Naibu waziri huyo imemuwezesha kuona namna miradi hiyo inavyotekelezwa pamoja na changamoto zilizopo.Changamoto hizo kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya huyo ni pamoja na baadhi ya miradi fedha zake kutotolewa na serikali na kuna baadhi ya miradi fedha zake zimepokelewa kilichobakia na utekelezaji na ukamilishaji wa miradi hiyo kwa wakati.

Katika taarifa ya Mamlaka ya maji na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) iliyosomwa na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo,Mhandisi Patrick Nzamba aliweka bayana kwamba Mamlaka hiyo imepokea zaidi ya shilingi milioni 700 kati ya shilingi bilioni 1,150,000,000/= kwa ajili ya kugharamia visima ambavyo havijawekewa miundombinu viweze kuwekewa ili uzalishaji wa maji uweze kuongezeka.

Hata hivyo Mhandisi Nzamba alizitaja baadhi ya changamoto zilizopo katika uendeshaji wa Mamlaka hiyo kuwa ni pamoja na deni kubwa la ankara za nyuma za nishati ya umeme kwa ajili ya uzalishaji wa maji.

Kwa mujibu wa Mhandisi Nzamba Mamlaka hiyo inadaiwa shilingi milioni 475 katika kipindi cha kuanzia januri hadi sept,mwaka 2017 hali inayosababishiwa wakati mwingine kusitishiwa huduma ya umeme wakati Mamlaka hiyo pia ikizidai taasisi za serikali ambapo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana,taasisi hizo zilikuwa zikidaiwa shilingi 243,065,937.07/=.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: