Dogo Janja na Uwoya.

DAR ES SALAAM: Baada ya kusambaa kwa madai kuwa muigizaji Irene Uwoya amenasa ujauzito, imeelezwa kuwa mrembo huyo amejificha nyumbani kwa Video Queen matata Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ kukwepa kamera za mapaparazi.
Awali, mtoa ubuyu makini alilitonya Amani kuwa licha ya kuwa mrembo ‘aliigiza ndoa’ na msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ lakini kiuhalisia wanabanjuka kweli penzini hivyo bwa’mdogo huyo ndiye mhusika wa ujauzito huo.

“Kweli ile ndoa ilikuwa ni ya kwenye Tamthiliya ya Sarafu lakini bwa’mdogo alikuwa anapiga kweli sasa nasikia ndiyo hivyo tena kampa ujauzito,” kilisema chanzo hicho.
Kikizidi kushusha ubuyu huo, chanzo hicho kilidai kuwa Uwoya amekuwa akikwepa mapaparazi kwani anaona kama litakuwa ni jambo la aibu kwani uhusiano wao hakupenda uwe wazi.

“Si unajua Uwoya tangu awali alikuwa hapendi kuonesha kwamba ana uhusiano na Dogo Janja na ndiyo maana alikuwa akisema kuwa hana uhusiano naye licha ya Dogo Janja kudai amemuoa kweli Uwoya,” kilisema.
Makachero wa OFM walifika nyumbani kwa Uwoya, maeneo ya Sinza Mori na kuambiwa na majirani kuwa siku za karibuni, hawajamuona mrembo huyo nyumbani hapo.

“Hebu jaribuni kwa Masogange maana nasikia ndiyo kajificha huko,” kilisema chanzo hicho ambacho kilisema hakikusikia habari hizo za kwamba ni mjamzito.
Mapema wiki hii, makachero wa OFM walifika nyumbani kwa Masogange, maeneo ya Makongo Juu na kumkuta mfanyakazi wa ndani ambaye alikiri kuwa Uwoya yupo.


Siku iliyofuata, Masogange alipoulizwa kuhusu suala la kumficha Uwoya nyumbani kwake, alieleza jambo la tofauti na yule dada wa kazi aliyesema Uwoya kalala, akadai huwa anakwenda tu kumsalimia na kuondoka.
Alipotafutwa Dogo Janja ili kujua kama kweli mzigo ni wake, aliomba atafutwe Uwoya mwenyewe azungumzie suala hilo.
“Mimi niombe mumtafute Uwoya mwenyewe azungumze.”
Alipoulizwa Uwoya kuhusu suala la ujauzito na kujificha nyumbani kwa Masogange alikanusha na kusema si kweli kwani anaishi kwake.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: