Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewataka wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuhakikisha inakamilisha ukarabati wa shule za Jangwani na Azania kabla ya Januari 22, mwaka huu ili kuwezesha masomo kuanza.
Waziri Ndalichako ametoa
agizo hilo leo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kukagua Maendeleo ya ukarabti wa shule hizo.
Waziri ndalichako amesema ameridhishwa na namna ukarabati wa shule hizo unavyofanyika, licha ya kuwa bado kuna kazi kubwa ambayo bado haijafanyika.
Waziri ameitaka TBA kuhakikisha wanakamilisha miundombinu muhimu mapema ikiwemo madarasa, mabweni, na vyoo ili kuwawezesha wanafunzi kuanza masomo kabla ya januari 22, mwaka huu.
Kwa upande wake Msanifu Majengo Cecilia Muhongo wa TBA amesema wamejipanga kuhakikisha ukarabati wa miundombinu muhimu itakayowawezesha wanafunzi kuanza masomo inakamilika mapema.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
17/1/2018
Post A Comment: