Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amerejea tena jijini Dar es Salaam akiwa na kikosi chake cha Simba tayari kwa mechi ya kesho dhidi ya Singida United.

Simba imerejea Dar es Salaam na moja kwa moja kujichimbia kambini kwa ajili ya kusubiri mechi hiyo kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Okwi ambaye alijiunga na Simba juzi kabla ya kufanya mazoezi jana, ni kati ya wachezaji wanaotarajiwa kucheza mechi hiyo ya kesho, timu hizo zikikutana kwa mara ya kwanza baada ya Singida United kurejea Ligi Kuu Bara.

Simba inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 26 na Singida ina pointi 23 ikitaka ushindi ili kuhakikisha inaifikia Simba na ikiwezekana, kuipita.

MATOKEO SIMBA:
Simba 7-0 Ruvu 
Azam 0-0 Simba 
Simba 3-0 Mwadui
Mbao 2-2 Simba 
Stand 1-2 Simba 
Simba 1-1 Mtibwa 
Simba 4-0 Njombe
Yanga 1-1 Simba 
Mbeya 0-1 Simba 
Prisons 0-1 Simba 
Simba 1-1 Lipuli   


Ndanda 0-2 Simba 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: