VIDEO Queen anayekuja juu kwenye Bongo Fleva, Lulu Eugen ‘Amber Lulu’ ameshtuka kusikia mwanamuziki maarufu wa Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’ ambaye ni mpenzi wake kuwa amemmwaga na kumtambulisha mwanamke wake mwingine kwenye siku yake ya kuzaliwa.

Amber haamini kama mpenzi wake huyo amempiga kibuti na ni kama kweli atakuwa amepata mwanamke mwingine, basi atakuwa amemdhalilisha mno ukizingatia Prezzo alikuwa tayari ni mwanaume ambaye alishamweka moyoni mwake.

“Hilo la kutambulisha mwanamke mwingine nimelisikia, lakini kama ni kweli amemtambulisha mwanamke mwingine, atakuwa amenikosea kwa sababu yeye alikubali nimtambulishe hadi kwa ndugu zangu na nilishamweka moyoni,” alisema Amber Lulu
Share To:

msumbanews

Post A Comment: