HATIMAYE beki wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe ameingia kwenye kikosi cha wachezaji 18 watakaocheza dhidi ya Kagera Sugar leo
Kapombe hajawahi kuingia kwenye orodha ya wacheza 18 wa mchezo tangu aliposajiliwa na Simba mwezi Julai mwaka Jana.
Beki huyo wa zamani wa Azam amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi 5 akiuguza majeraha mbalimbali, jambo ambalo limemfanya ashindwe kuitumikia timu yake hiyo mpya.
Wakati huo huo, kiungo Said Ndemla ameingia kwenye kikosi cha kwanza leo baada ya kuonyesha kiwango bora dhidi ya Singida United.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: