Mkazi mmoja wa Dodoma anayejitangaza kama nabii, Tito Machija amesema watu wasimuona kuwa hana akili kutokana na mahubiri yake ambayo yanatofautiana kwa kiasi kikubwa na imani za waumini wa dini nyingine, hasa Wakristo.
Machija, ambaye anajulikana kama ‘Nabii Tito’ anahamasisha kuoa mke zaidi ya mmoja, ikiwa ni pamoja na kutembea na wafanyakazi wa ndani; anatumia pombe kunasa waumini na anadai hataki nyimbo za injili kwenye ‘ibada’ zake, ambazo nyingi hufanyikia baa.
‘Nabii’ huyo anaonekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa amevalia kanzu nyeupe yenye misalaba miwili, chupa ya bia na kitabu kitakatifu aina ya Biblia.
“Nawashangaa wanaoniona mimi sina akili, niko timamu kabisa na ninaelewa ninachokifanya,” alisema 
“Narudia tena kusisitiza kuwa walevi ndio watakaoingia ‘mbinguni’ na mafundisho ninayoyatoa ni sahihi,”
Share To:

msumbanews

Post A Comment: