Na Jerry C. Muro
Mkuu wa  Mkoa wa  Ruvuma Mhe Christina Mndeme akiwa ameshika moja ya gunia la serikali yaliyokamatwa kwenye ghala binafsi la  Lotary Nkondola eneo la  Ruhuwiko Songea.

Tukio hili limetokea Leo asubuhi kufuatia ziara ya ghafla NFRA kanda ya Songea kufuatia tuhuma za watumishi wa  *NFRA* kuiba mahindi tani  30 toka maghala ya serikali hapo Desemba 2017.

Katika Picha wa kwanza kulia  ni Meneja wa  NFRA Songea Amos Mtafya (mwenye shati la  drafti) na katikati ni  Mkuu wa  wilaya ya Songea Pololet Mgema.

Kwenye tukio hilo mkuu wa  Mkoa Mhe Mndeme ameagiza kukamtwa kwa meneja huyo  pamoja na watumishi wenzake Lugano Moses (Mhasibu) na Mariam  Mpangala ( Afisa Maghala) pamoja na wafanyakazi wa  ghala binafsi wanne.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: