Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta (kati kati) akisoma jiwe la msingi mara baada ya ufunguzi rasmi wa tawi jipya la NMB Mto wa Mbu lililopo katika Wilaya ya Monduli. Hafla hii ya Uzinduzi imefanyika mwishoni mwa wiki. Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini –Salie Mlay pamoja akishuhudia tukio hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta (kati kati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi jipya la NMB Mto wa Mbu lililopo katika wilaya ya Monduli . Hafla hii ya Uzinduzi imefanyika mwishoni mwa wiki. Kwanza kulia ni Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini –Salie Mlay pamoja na Meneja wa NMB Tawi la mto wa Mbu wakishuhudia uzinduzi huo.
……………………………………………………………………..
“Nawapongeza sana NMB wamefanya huduma za kipenki kuwa rahisi kuliko kitu chochote kwangu. Nikihesabu nimara ngapi nimekwenda benki kwa mwaka mzima haitofika hata mara tano. Lakini natumia huduma za kibenki kila siku. Ninajivunia kuwa mteja wa NMB. Natumia simu yangu kufanya miamala tofauti tofauti na inanisaidia kutumia muda wangu vizuri..NMB Mobile imekua mkombozi wangu na hata kwa wengine pia. Kwa kweli NMB mnastahili pongezi juu hili kwa kua NMB Mobile imekua mkombozi wa Muda pia….” Alisema Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo alipozindua Tawi la NMB Ngaramtoni.
NMB imezindua matawi mengine mapya matatu katika mikoa ya kaskazini ikiwapo Moshi na Arusha. Hii ni moja ya jitiahada zinazofanywa na uongozi wa benki ya NMB ili kuhakikisha kwamba huduma za benki zinamfikia kila mwananchi kwa ukaribu na uharaka wa huduma za kibenki.
Wiki iliyopita kwa mfululizo benki imezindua tawi la NMB Mbuyuni lililopo katika Manispaa ya Kilimanjaro na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Anna Mghwira alizinua tawi hili, Tawi la NMB Ngaramtoni lilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo. Tawi hili lipo katika Mkoa wa Arusha Wilaya ya Arumeru pamoja na Tawi la NMB Mto wa Mbu tawi hili lipo ndani ya mkoa wa Arusha katika Wilaya ya Monduli na Mgeni rasmi alikua Mhe. Iddy Kimanta Mkuu wa Wilaya ya Monduli.
Matawi haya yote ni mapya kabisa na yatatoa huduma za kibenki kama Matawi mengine ya NMB Matawi haya yote matatu yamekua neema kubwa sana kwa wakazi wa wilaya hizi kutokana na adha waliyokua wakiipata awali ya kwenda katika wilaya nyingine za jirani ili kupata Huduma za kibenki.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti wateja wa NMB walisema kwamba haikua kazi rahisi kwao kusafiri mwendo mrefu wakiwa wamebeba pesa nyingi baada ya kuwa wameuza mifugo na mazao yao kwenye minada mbalimbali. Kuna mfanyabishara mwenzetu wiki iliyopita alinusurika kuibiwa fedha zake karibu kabisa na dukani kwakwe. Tatizo lake alikuwa anaweka mauzo yake ya zaidi ya wiki anaweka kwenye ndoo ndani ya duka lake. Inapofika wiki mbili ndipo anapeleka fedha zake benki. Sasa hivi NMB wapo hapa karibu halafu pale pale karibu Sokoni kuna wakala wa NMB. Imekua rahisi sana kwetu hatutarajii kusikia tena habari za wafanyabiashar akuibiwa tena. Tunawashukuru sana NMB kwa kujua hitaji letu la muda mrefu….Alisema Elibariki Kimario Mkazi wa Moshi mjini.
Uzinduzi wa matawi haya matatu katika mkoa wa kilimnajaro na Mkoa wa Arusha unafanya NMB kua na matawi zaidi ya 2012 nchi nzima pamoja na Mashine za kutolea fedha zaidi ya 800 Mawakala 4100 nchi nzima. Ni kusudio letu kwamba tuweze kuwafikia wateja wetu kila mahali walipo na wasipoteze muda mwingi kupata huduma za Kibenki. Alisema Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker wakati wa uzinduzi wa tawi la NMB Ngaramtoni.
Sehemu ya wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba mbali mbali zilizokua zinaendelea wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la NMB Mto wa Mbu lililopo katika Wilaya ya Monduli. Hafla hii ya Uzinduzi rasmi imefanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya tawi la NMB Mto wa Mbu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: