www.msumbanews.blogspot.com
DIWANI wa kata ya Buigiri Wilaya ya Chamwino Keneth Yindi amewataka vijana kutumia fursa walizokuwanazo za ujana katika kuisaidia serikali kuinua uchumi wake ikiwemo wa kijamii na kiroho.

Yindi amesema hayo alipokuwa akizungmza na vijana wa kanisa la Anglikan parishi ya maili mbili Dodoma kwenye harambe ya kuchangia uziduzi wa albamu.
Amesema vijana wanayo nafasi kubwa ya kutumia fursa zilizopo katika kuinua uchumi wa Tanzania na hatimaye kuleta maendeleo,badala ya suala hilo kuachia serikali na wadau wengineo wakiwemo taasisi za kidini.

Diwani huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa habari uchapishaji na matangazo kutoka Umoja wa Madhehebu ya Kikristo Mkoa wa Dodoma,aidha amewataka vijana kujishughulisha na miradi mbalimbali ili waweze kuondokana na utegemezi katika suala la maendeleo.

Amesema baadhi ya vijana walio wengi wahajitumi na muda mwingi wanautumia kwa kukaa vijiweni huku wakisubiri kufadhiriwa hali ambayo imewasababishia kujikuta wakutumiwa na shetani kwa kufanya matendo maovu.

Akizungumza na vijana wa kanisa hilo la Anglikana kwenye uzinduzi huo,amewataka pia kutumia nafasi zao kuisaidia serikali katika kuhubiri neno la mungu kwa wezao ambao bado wanaendelea kufanya kutenda vitendo visivyo halali.

“Tumieni muda wenu kuisaidia serikali katika kuhubiri habari njema za Mungu kwa vijana wezenu ambao bado wanatumikishwa na shetani na kusababisha kuchukiwa na jamii inayowazunguka na hata kwa serikali pia”alisema.

Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa Madhehebu ya dini mkoa wa Dodoma,Dkt Elia Mauza amewataka vijana kwa upande wao kuhakikisha wanaiombea serikali ya awamu hii ya tano ili fursa zilizopo ziweze kuwafikia watanzania wote.

Amesema jukumu la kuiombea Taifa na viongozi waliopo halipo tu kwa madhehebu ya dini na baadhi ya watu,bali lipo hata kwa vijana ambao wanaoelezwa kuwa ndiyo wenye nguvu kwa mujibu wa vitabu vitakatifu vya Mungu.
Mwisho.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: