WAFANYABIASHARA DODOMA KUIJENGA DODOMA .
MKUU
wa wilaya ya Dodoma mjini Christina Mndeme amewataka wafanyabiashara waliomo
mkoani humo kuijenga makao makuu ya nchi
kwa kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya
biashara kama nyumba za makazi vikiwemo viwanda na mashamba badala ya kusubiri watu
kutoka nje kuja kuwasaidia kuwekeza
Mkuu
wa wilaya aliitoa kauli hiyo wakati alipokuwa
akiongea na wafanyabiashara wa viwandani na mashambani walio na
wasiokuwa ndani ya [TCCIA] waliokuwa wamekutana kwa lengo la kuzijadili
fulsa na
changamoto zitakazokuwepo kutokana na serikali kuhamia mkoani Dodoma
linalotokana na tamko la hayati Julias Kambarage Nyerere alilolitoa
mwaka 1972
kuwa makao makuu ya nchi yahamishiwe mkoani humo
Mndeme
alizitaja Fulsa zinazotokana na ujio wa makao makuu mkoani humo kuwa ni ujenzi
wa nyumba za makazi, jengo la kisasa la biashara ambalo litakuwa na gorofa 5
litakalojengwa eneo lilipo soko la sabasaba na kituo cha biashara
kinachotarajiwa kujengwa Ihumwa ambako patajengwa bandari kavu na tayari hekari
500 zimetengwa
Pia
kijijini hapo pametengwa hakari 217,000 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa yenye standard Gage pia stendi
kuu ya mabasi ya kwenda mikoani ambayo itajengwa katika eneo linalotazamana na
viwanja vya maonyesho ya nane nane wanasubiliwa
wawekezaji ambao watajenga vibanda vya biashara, migahawa na maduka
makubwa, huku viwanja hivyo vya nanenane vikitakiwa kuboreshwa ili shughuli za
kibiashara ziweze kufanyika mwaka mzima tofauti na sasa ambapo baada ya
maonyesho ni magereza na JKT pekee hubakia wakifanya shuhuli zao
Alisema
katika eneo la uwekezaji la Njedengwa patajengwa Kiwanda cha kusindika zabibu
kwa ajili ya kutengeneza Mvinyo, Juice ikiwa ni pamoja na kuzikausha
kunakoambatana na eneo la kilimo cha zao hilo kutengwa katika kijiji cha Gawaye
kwa jumla ya heka 600, pia ujenzi wa kiwanda cha kusindika mazao ya mifugo
yakiwemo maziwa fresh, mtindi na hata soseji ambazo zitakuwa zikitokea Dodoma
na kusambaa nchi nzima na hata nje ya nchi
“sasa
hivi tuna wakazi 410,000 na baada ya makao makuu kukamilika idadi ya watu
itaongezeka hivyo tumieni fulsa hii kuwekeza ninyi wafanyabiashara wa hapa kwa
kile mnachokiweza ili isijefikia wakati ambapo wanaweza kuwekeza watu kutoka
nje halafu mkabaki kulalamika kwa nini nisingekuwa mimi na hapo utakuwa
umechelewa”, alisema
Post A Comment: