Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda akitoa maelekezo kwa wajumbe wa kamati ya Siasa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo wakati wakikagua moja ya caravati linalojengwa katika Barabara ya Maluga Mtaa Saba -Misuna na Mgungia hadi Kaselya wakati kamati hizo zilipokuwa zikikagua  miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake Tarafa ya Shelui wilayani humo jana.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iramba, Samuel Ashery akizungumza wakati kamati hizo zilipokuwa zikikagua mradi wa maji wa Kijiji cha Wembere uliopo katika Tarafa hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi akizungumza kwenye ziara hiyo.
Afisa Tarafa ya Kinampanda Cholo Mtaki akiwatambulisha viongozi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kitukutu wakati wa ziara ya kamati hizo.
Meneja wa Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Iramba Mhandisi Ezra Mwacha akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa maji wa Kijiji cha Wembere.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Misigiri akitoa taarifa ya mradi wa vyoo na uwekaji wa miundombinu ya maji katika zahanati hiyo.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kitukutu Dada Kazimoto akizungumza mbele ya kamati hiyo.
Ukaguzi wa tenki la maji katika zahanati hiyo ukifanyika.
Diwani wa Kata ya Ulemo akichangia jambo kwenye ukaguzi wa mradi huo wa vyoo.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Ulemo Luka Kasanga akitoa taarifa ya ujenzi wa zahanati hiyo.
Muonekano wa zahanati hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akichangia jambo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa zahanati hiyo ya Ulemo.
Muonekano wa bweni la Wasichana wa Shule ya Sekondari ya Tumaini baada ya ujenzi wake kukamilika
Wajumbe wa kamati hizo wakipokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Wasichana ya Tumaini, Mwalimu Zainabu Mtinda ya kukamilika kwa ujenzi wa bweni katika shule hiyo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya KengyegeMwalimu Emmanuel Twiyogehe akitoa taarifa ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Maluga.
Muonekano wa baadhi ya majengo yanayoendelea kujengwa Shule mpya ya Maluga.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa shule hiyo mpya ya Maluga.

Mkzi wa Kijiji cha Maluga akiishukuru Serikali na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa shule hiyo.
Diwani wa Kata ya Maluga akichangia jambo kuhusu ujenzi wa shule hiyo.
Wajumbe wa kamati hizo wakikagua ujenzi wa shule hiyo.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa shule hiyo.


Mkutano wa hadhara ukiendelea Kijiji cha Kitukutu.
Mkutano ukiendelea.Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Iramba Michael Abbas akizungumza wakati akiwatambulisha viongozi wa chama hicho kwenye mkutano huo.

Katibu wa CCM wa Wilaya ya Iramba, Comrade Ephrahimu Kolimba akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya hiyo Mr Mwajala akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo aliwahimiza Wazazi na Walezi kuhamasika kuchangia chakula cha wanafunzi wakiwa shuleni.


Mkaguzi wa mradi wa maji wa Kijiji cha Wembere ukifanyika.
Muonekano wa mradi huo wa maji wa Kijiji cha Wembere.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Wembere Eliud Mbogo akiishukuru Serikalikwa kuwapelekea mradi huo.
DC Mwenda akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi huo wa maji.
Makofi yakipigwa kufurahia mradi huo.
Ukaguzi wa ujenzi wa Kituocha Afya cha Umtoa ukiendelea.
Muonekano wa baadhi ya majengo yanayoendelea kujengwa ya Kituocha Afya Mtoa
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mtoa, Sori Abushehe akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho.
Muonekano wa chumba cha maabara ya Shule ya Sekondari ya Mtoa kinachoendelea kujengwa.Ukaguzi wa ujenzi wa maabara hiyo ukiendelea

Meneja wa TARURA wa wilaya hiyo Venance Kibona akitoa taarifa ya ujenzi wa Barabara ya Shelui kwenda Tintigulu.
DC Mwenda akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nselembwe wakati wa ukaguzi wa barabara hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda pamoja na wajumbe wa kamati hizo wakisaidia kuchanganya mchanga wa ujenzi wa nyumba ya watumishi wa Kituo cha Afya Shelui.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Shelui, Alex Mpwenku akitoa Taarifa ya ujenzi wa nyumba ya watumishi wa kituo hicho.
Ujenzi wa kituo hicho ukiendelea.Mkutano wa hadhara Kijiji cha Nselembwe ukifanyika.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.Baadhi ya wajumbe hao wakiwa kwenye mkutano Kijiji cha Nselembwe Shelui.
Diwani wa Kata ya Shelui akichangia jambo kwenye mkutano huo.

 


Na Dotto Mwaibale, Singida.


MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda ametoa mwezi mmoja kwa Wazazi na Walezi wa wanafunzi 16 wa Tarafa ya Shelui ambao hadi sasa hawajaripoti shuleni baada ya kufaulu darasa la saba kwenda Sekondari kuhakikisha wanafanya hivyo na atakae kahidi agizo hilo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Mwenda ametoa agizo hilo jana  wakati akiwahutubia  Wananchi wa Tarafa ya Shelui kwenye mkutano wa hadhara baada ya  kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo  kumaliza kukagua miradi ya maendeleo iliyopo katika Tarafa hiyo.

"Serikali haiwezi kuvumilia kuona wanafunzi waliofaulu kwenda kuanza Sekondari hawaendi shuleni licha ya kutumia fedha nyingi ya kuboresha mazingira bora ya kupata elimu hivyo naagiza kuanzia leo Machi 30, 2022 hadi ifikapo  Aprili 30, 2022 watoto hao wawe wamepelekwa kuanza masomo na wazazi watakao kahidi agizo hilo tutawachukulia hatua kali" alisema Mwenda.

Akizungumzia ukaguzi wa miradi hiyo iliyogharimu zaidi ya Sh.9  Bilioni alisema kamati hizo zilifanya ukaguzi huo ili kuona nini kimefanyika katika mwaka mmoja wa uongozi wake Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ametoa fedha nyingi  kwa ajili ya kutekeleza miradi katika Tarafa hiyo ambapo waliridhishwa na utekelezwaji wake.

Alisema baada ya kuiona walipanga kufanya mkutano huo wa hadhara ili kuwaeleza wananchi  mafanikio makubwa ya utekelezaji wa miradi hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu kuwa madarakani.

Akizungumza kwa nyakati tofauti  katika ziara hiyo Mwenda alisema miradi hiyo inafanyika ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) na Serikali inawajibu wa kuikagua ili kuona kama inatekelezwa kwa viwango vinavyo kubalika.

Alisema  Serikali inatumia fedha nyingi kuitekeleza akitolea mfano ujenzi wa madarasa yaliyotokana kwa fedha za mradi wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid-19 ambayo yamewaondolea adha kubwa ya michango wananchi ya kuchangia ujenzi na ununuaji wa madawati.

Mwenda  alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo na kuwaomba viongozi ilipo miradi hiyo kuwahamasisha wananchi wao kuitunza.

Aidha Mwenda aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa vijana wanaoshiriki katika zoezi la anuani za makazi na postikodi linaloendelea nchi nzima kwa kuwaelekeza majina ya mitaa na mambo mengine yanayohitajika na akawaomba kufanya hivyo pia katika zoezi la Sensa ya watu na makazi.

Mwenda aliwapongeza wananchi wa Tarafa hiyo kwa kuitikia katika kilimo ambapo mazao mengi yanaonekana kustawi ambapo aliwataka kujiadhari na walanguzi ambao wameanza kupita kwa wakulima kuwashawishi ili wanunue mazao yao yangali shambani kwa bei ya ulanguzi.

Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Samuel Ashery aliwaomba wananchi ilipo miradi hiyo kuitunza na akawataka wakandarasi kuikamilisha kulingana na thamani ya fedha walizopewa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Innocent Msengi aliwaomba wakandarasi waliopewa kuijenga miradi hiyo kuijenga kwa wakati kama walivyo kubaliana kwenye mikataba ili wananchi waweze kuanza kuitumia kwa wakati.

Baadhi ya  miradi iliyokaguliwa na kamati hizo  ni ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Maluga kwa gharama ya Sh.470 Milioni, ujenzi wa  bweni moja kwa ufadhili wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Tumaini aambao  uligharimu Sh.75 Milioni, ukamilishaji wa Jengo la Zahanati ya Ulemo ambapo walipokea Sh.50 Milioni na ujenzi wa mradi wa wa vyoo na uwekaji wa miundombinu ya ya maji ndani ya Zahanati ya Misigiri kwa gharama ya Sh. 25.2 Milioni.

Miradi mingine iliyokaguliwa ni ujenzi wa barabara za Maluga-Mtaa wa Saba, Mtaa saba- Misuna na Mgungia-Kaselya kwa gharama ya Sh.492,019,500 fedha zilizotoka Serikali Kuu, ujenzi wa mradi wa nyumba za Watumishi katika Zahanati ya Shelui kwa gharama ya Sh.90,000,000 ambao unahusisha jengo moja lenye nyumba tatu za watumishi, ujenzi wa Kituo cha Afya Mtoa ambacho kitagharimu Sh.400,000,000 na  ukamilishaji wa vyumba viwili vya maabara Shule ya Sekondari Mtoa.

Mwenda alitaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa mradi wa maji Kijiji cha Wembereambao umetengewa bajeti ya Sh. 356,080,529 na matengenezo ya barabara ya Shelui kwenda Tintigulu. 


Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: