Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kenani Kihongosi, amewaomba wananchi wa Jimbo la Ngorongoro Mkoani Arusha, kutokubali kurubuniwa na wanasiasa wenye uchu wa madaraka wanaopita maeneo yao ya mjini bila kwenda vijijini kuomba kura, badala yake wamchague Emmanuel Shangai wa Chama cha Mapinduzi CCM.


Kauli hiyo ameitoa hii leo wakati akimnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya (CCM),  katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Kapenjiro katika Kata ya Nayobi Wilayani Ngorongoro.

 Kihongosi ameeleza kuwa Chama cha Mapinduzi CCM ndicho chama pekee kitakachowakomboa wana Ngorongoro katika shida mbalimbali zinazowakabili kama maji, umeme, afya, elimu na miundombinu ya barabara. 

 Amesema CCM ndicho chama pekee chenye Ilani ya uchaguzi inayotekelezwa kwa sasa hivyo, ni muhimu wananchi wakamchagua mgombea anayetokana na Chama tawala ili waendelee kutatuliwa kero mbalimbali zilizo katika maeneo wanayoishi.

 “Wapinzani hawana ilani, hawana ofisi, kwa ngazi za kijiji, kata, wilaya, mkoa na Taifa, sasa mkiwachagua mkipata shida, mnakwenda kuwapata wapi, msirubuniwe na watu wasiojulikana wenye uchu wa madaraka, chagueni mgombea wetu mwenye Ilani bora ambayo iko kazini,” amesema

 Kihongosi ameeleza kuwa mgombea wa CCM ana uwezo wa kuwasiliana na viongozi mbalimbali wa kitaifa kama Rais na Waziri Mkuu na akasilizwa shida zake kwa wakati, lakini wa upinzani hawezi kupata nafasi hiyo, wasijaribu kumchagua kwa sababu hana mtu anayekwenda kufanya naye kazi bungeni.

“Sasa wanaomba ubunge na ilani ya uchaguzi inayotekelezwa hawana, msiwachague, wanataka kwenda kujinufaisha kwa maslahi yao binafsi, CCM imemleta Shangai. “Amepimwa na vikao vyote vya juu, ameonekana anafaa, mpeni kura akaendelee kusimamia maendeleo yenu,” amesema Kihongosi. 

Naye Mgombea Ubunge Emmanuel Shangai amesema kuwa, kama atapata ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo, atahakikisha kero zinazowakabili wananchi, zinapatiwa ufumbuzi wa haraka ili waendelea na shughuli za kila siku pasipo vikwazo. 

“Bado jimbo letu lina changamoto nyingi ambazo zinahitaji kutatuliwa, naombeni kura zenu ili niweze kuwatumikia, nawaahidi katika uongozi wangu, hakuna mwananchi wala mtumishi atakayenyanyaswa na mtu mwingine, nitawatumikia kwa weledi na uaminifu mkubwa,




















Share To:

Post A Comment: