Na Asila Twaha, Morogoro


Timu ya TAMISEMI Sports Club imeanza vyema Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za serikali SHIMIWI yanayofanyika Kitaifa Mkoani Morogoro kwa kuichapa timu ya Ras Dar es salaam magoli 2-0.


Mchezo huo ulichezwa majira ya saa 8 za mchana katika uwanja wa shule ya sekondari  Morogoro ambapo awali timu hizo zilicheza kwa tahadhari kubwa na mpaka wanaenda mapumziko hakuna aliyeweza kumfunga  mwenzake.'


Kipindi cha pili timu ya TAMISEMI Sports Club ilibadili mchezo wakishambulia kwa kasi na kufanikiwa kupata bao kutoka kwa mchezaji wao machachari Lewis Mwasekaga baada ya kumzidi Mlinzi wa Ras Dar es Salaam na kuachia shuti kali lililokwenda moja kwa moja nyavuni.


TAMISEMI Aports Club haikuishia hapo iliendelea kulisakama lango la Ras Dar es Salaam kwa mara nyingine tena Mwasekaga alirudi kambani kwa shuti kali lilimshinda mlinda lango na kuiandikia timu yake bao la pili.


Mpaka filimbi ya mwisho ya mwamuzi inapulizwa timu ya Ras Dar es Salaam imekubali maumivu ya kichapo kutoka kwa timu ya TAMISEMI Sports Club.


Baada ya mchezo huo nahodha wa timu ya TAMISEMI Sports Club Abubakari Saidi amesema mchezo ulikuwa mgumu lakini walijituma kwa kucheza kwa bidii dhidi ya wapinzani wao kupata ushindi na kuwashukuru waamuzi kwa kuchezesha mchezo huo kwa busara.

Kwa upande wake kocha wa timu hiyo Charles Luhende amesema baada ya mechi ya leo wanakwenda kujianda kwa mechi inayofuata kwa ajili ya kuendeleza ushindi walioupata.

Share To:

Post A Comment: