Tuesday, 19 October 2021

RAIS AZINDUA MRADI WA MAJI LONGIDO, DC ASEMA MAPATO NAMANGA YAMEPANDA.

 Na Lucas Myovela_ Arusha

Longido. Mapato katika mpaka wa Namanga unaotenganisha Tanzania na Kenya, yamepaa na kufikia Sh33 bilioni ndani ya miezi sita.

Mkuu wa wilaya ya Longido, Nurdin Babu ametoa taarifa hiyo leo Oktoba 18 kwa Rais Samia Suluhu ambaye yupo katika ziara ya siku moja wilayani hapa.

Babu amesema katika kipindi cha miezi sita, mpaka huo ulikuwa umepangiwa kukusanya kiasi cha Sh30 bilioni.

"Ukisanyaji mapato unakwenda vizuri hapa mpaka wa Namanga, watu wanalipa Kodi vizuri," amesema

Akizungumzia elimu amesema wilaya hiyo, wilaya imepokea kutoka Serikalini Kiasi cha sh Bilion 1.4 ambazo zinakwenda kumaliza matatizo ya sekta ya Elimu katika wilaya hiyo.


Mbunge wa Jimbo la Longido, Stephen Kiluswa alimshuru Rais Samia Kwa uzinduzi mradi mkubwa wa maji katika wilaya hiyo ambao unakwenda kutatua shida ya maji.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema  watendaji wa wizara  hiyo hawatakuwa  kikwazo kwa Watanzania kupata maji safi na salama na ya kutosheleza.

Waziri huyo ametoa ahadi hiyo leo Oktoba 18, 2021 mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji Longido, Arusha.

Waziri huyo amemshukuru Rais Samia kwa niaba ya watendaji wa wizara hiyo kwa kuendelea kuwaamini viongozi wa kuu katika sekta hiyo, akijitolea mfano mwenyewe kwamba tangu alipomaliza chuo kikuu kazi yake ya kwanza ni Ubunge.

“Sikuwahi kufanya kazi popote lakini wewe na Hayati John Magufuli mliniamini kuwa Naibu Waziri wa Maji na leo Waziri wa Maji sio jambo jepesi, familia yangu mama yetu ni mama ntilie kabisa lakini umeniamini na kunipa dhamana hii kubwa,” amesema

Amesema wakati anateuliwa, Rais Samia alimuita Ofisi kwake na kumueleza baadhi ya mambo ikiwemo kumsikiliza na kumuelewa kwamba sehemu zote alizopita changamoto kubwa aliyokutana nayo ni maji.

“Waathirika wakubwa ni akina mama na wanatembea umbali mrefu, wakati huo baba wamemuacha nyumbani akihitaji maji na kuoga lakini hawajuhi maji yanapatikana wapi na ndoa nyingi zinateteleka kwa sababu ya ukosefu wa maji,” amesema Aweso.

Waziri huyo amemueleza Rais Samia utekelezaji wa miradi unategemeana na fedha na anaishukuru serikali imekuwa ikitoa fedha kuhakikisha miradi yote inakamilika.

Amesema mradi huo wa Longido umetekelezwa kwa Sh15.8 bilioni fedha hizo ni za ndani ambazo wananchi wamekuwa wakilipa kodi na wala sio za mkopo.


No comments:

Post a Comment