Friday, 8 October 2021

Mhandisi Mahundi atembelea vyanzo vya maji vya bonde la maji mto RufijiNa Mwandishi wetu,Kilombero


NAIBU  waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amewasili Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro na kupokelewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya hiyo ndugu Ebeneza Emmanuel.
Mheshimiwa Mahundi yupo Wilayani Kilombero kwa ajili ya ziara ya siku Moja ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea vyanzo vya Maji vinavyosimamiwa na Bodi ya Maji ya Bonde la Rufiji. 
Leo Octoba 7, 2021 ametembelea chanzo kilichopo katika Mto Kilombero.
Mto Kilombero ni moja ya chanzo ambacho kinachangia maji kwa zaidi ya asilimia 65 kupeleka maji kwenye bwawa la kufua umeme wa Maji la Mwalimu Julius Nyerere Hyro Power Project.

No comments:

Post a Comment